Makbuus Samak/ Makbuus ya Samaki (U.A.E)

Makbuus Samak/ Makbuus ya Samaki (U.A.E)

   

    

Vipimo

Mchele wa Basmati - 4 vikombe

Samaki  wa chango - 2 Wakubwa

Vitunguu vilivyokatwakatwa - 3

Samli au mafuta - ¼ kikombe

Buharaat (bizari ya Makbuus) - 2 vijiko vya supu

Bizari ya manjano (haldi/tumeric) - 1 kijiko cha chai

Nyanya zikizomenywa na kukatwakatwa - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu        

Loomi (ndimu kavu) au ya unga - ½  au ½ kijiko cha chai

Mdalasini kijiti - 1

Karafuu nzima - 3

Hililiki nzima - 4

Maji - 5 vikombe

Kotmiri iliyokatwakatwa - ½ kikombe

Chumvi - kiasi

 

Baharaat – Bizari Ya Makbuus

Pilipili Manga - ½ kikombe

Gilgilani (Corriander seeds) - ¼ kikombe

Mdalasini vijiti - ¼ kikombe

Karafuu - ¼ kikombe

Bizari ya pilau (cumin seeds) - 1/3 kikombe

Hiliki- 2 vijiko vya chai

Paprika ya unga - ½ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Baharaat (bizari)

Chambua hiliki utoe kokwa zake, kisha tia vitu vyote katika mashine ya kusagia (grinder) usage hadi iwe unga.

Changanya na Paprika bizari ikiwa tayar.

Ihifadhi katika chupa yenye mfuniko wa kubana vizuri.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Makbuus

Vipimo Vya Samaki:

Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Maji ya ndimu - 3 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki

 1. Changanya masala ya samaki katika kibakuli kisha mpake samaki vizuri na mwache kiasi robo saa akolee masala.
 2. Mchome (grill) samaki hadi aive huku ukimgeuza.
 3. Eupa weka kando.

Namna Ya kutayarisha  Na Kupika Wali

 1. Osha na roweka mchele kwa muda kiasi.
 2. Katika sufuria ya kupikia, tia samli au mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia baharaat na bizari ya manjano, kaanga kwa dakika moja hivi.
 3. Tia nyanya, karafuu, loomi, mdalasini, hiliki, changanya vizuri na endelee kukaanga.
 4. Tia maji (inategemea mchele unaotumia, huenda ukahitaji zaidi)
 5. Mwaga mchele maji uliyorowekea, mimina mchele katika supu, tia kotmiri, changanya vizuri, funika uchemke mchele, punguza moto na pika wali kama inavyopikwa pilau ukoroge mara moja au mbili tu.
 6. Ukishaiva wali, pakua katika sinia/sahani na weka samaki juu ya wali.
 7.  

Kidokezo: 

 1. Ukipenda badala ya kupika wali katika sufuria baada ya kutia mchele na kukaribia kuiva, na kabla ya kukauka supu yote, mimina katika treya ya jalbosi (Treya ya foil) upike ndani ya oveni (bake) kwa mtoto wa takriban 400-450º   kwa muda wa dakika 20-25.
 2. Baharaat hiyo inatumiwa katika vyakula vya nchi za Kiarabu (Gulf States), hivyo unaweza kutumia kupikia  makbuus ya vitoweo vingine kama nyama na kuku na vyakula vinginevyo kama michuzi n.k.

 

 

Share