Haliym Ya Nyama Ng’ombe Bokoboko La Ki Pakistani

Haliym Ya Nyama Ng’ombe Bokoboko La Ki Pakistani

 

Vipimo

Nyama ng’ombe bila mifupa - 1 kilo

Mifupa ya nyama ng’ombe - ½

Tangawizi mbichi ilosagwa au kukunwa -

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha kulia

Pilipili mbichi ilosagwa - 3

Shayiri - ¼ kikombe

Ngano - ¼ kikombe

Dengu za manjano za kupasuliwa - ¼ kikombe

Chooko za kupasuliwa -

Hadesi nyekundu

Hadesi za kijani

Mchele

Bizari ya paprika (nyekundu) - 1 kijiko cha chai

Gilgilani (dania/coriander) - 1 kijiko cha chai

Haldi (bizari manjano/kurkum) - ½ kijiko cha chai

Jira (bizari pilau/cumin) - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya kijani ilosagwa -

Karafuu ya unga -

Jani la bay (bay leaf) - 1

Majani ya mchuzi - 3-5

Chumvi

Samli - ½ kikombe

Vitunguu kaanga slaisi, chuja mafuta, vivuruge - 3

Kotmiri majani katakakata - Kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Osha na roweka aina zote za nafaka, hadesi, mchele na kadhaalika kwa muda wa masaa 5 au zaidi.
  2. Osha nyama na mifupa, changanya na bizari zote, chumvi, tangawizi ilosagwa na thomu.
  3. Weka samli katika sufuria, kisha tia nyama, kakaanga vizuri.
  4. Tia nafaka zote na maji yake, ongezea maji mengi, changanya vizuri kisha funika ichemke na ipikike kwa mto mdogo mdogo sana kwa muda wa masaa 5 au zaidi mpaka nyama yote ilainike kabisa na nafaka zake zote ziwe laini.
  5. Ikiwa maji yamekauka na vitu bado havikulainika ongezea maji.
  6. Toa mifupa utupe, changanya vizuri motoni, mpaka iwe kama bokoboko.
  7. Epua umimine katika bakuli, upambie vitunguu vilokaangwa na kotmiri na kamulia ndimu unapokula ukipenda.

 

Kidokezo

Unaweza kununua boxi la tayari la haliym kupata aina za nafaka, hadesi, na bizari yake.

Tolea kwa mikate ya naan ukipenda.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

Share