Ibiliys Anamwandama Na Ana Maneno Ya Kufru Moyoni Mwake, Afanyeje?

SWALI:

 

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh, baada ya maamkizi haya ya kiislaam inshaallah Mwenyezi Mungu Subhaana Wa Taala awalipe mema hapa duniani na huko akhera

Sheikh huyu ni iblisi au nafsi inayonikufurisha.Mwezi wa Ramadhani ilinijia maneno ya kufru sijayatamka kwa maneno lkn moyo uliyatamka baadae hujuta na kuomba maghfira kwa Allah lkn bado nina wasiwasi mpaka hivi leo na Mashaallah SHEIKH najitahidi alhamdulillah kujikinga na nyiradi sahihi zilizomo ktk hiswnu muslim na mpangilio wa kusoma qur ani kila baada ya swala ya alfajiri na pia nikigutuka humkumbuka Allah nje ya swala na dua

mbali2 husoma za kinga na yote haya nayafanya kwa ikhlasw Sheikh   nakumba nifanye nini tena ili niondokane na kufru hizi


 

JIBU:

 

Sifa zote njema zamstahikia Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Fikra zote zinazokujia hakikisha kuwa hudumu nazo na wala huzipi nafasi kukaa katika moyo wako kwani Shaytwaan huwa anakutia wasi wasi na kukuletea fikra za namna hii au ile ambazo zote ni kinyume na Dini yako.

Shaytwaan huenda akakupa fikra kuwa Mola wako yuko namna hii au ile au fikira yoyote ile yenye kuonekana kama ni ukafiri, wewe unachotakiwa ni kuelewa kuwa hayo ni katika wasi wasi anaoutia Shaytwaan katika nyoyo za Waumini na muombe Allaah Akuondoshe na Akuepushe na fikra hizo na kama hizo. Hakikisha vilevile kuwa moyo wako hauathiriki na fikra hizo, Allaah Anasema katika Qur-aan:

Bali anakushikeni kwa yanayochuma nyoyo zenu. Na Allaah ni Mwenye kusamehe na Mpole.” Al-Baqarah: 225.

 

Kadhalika jiepushe na faragha mara zote, kwani faragha ndio mara nyingi huleta fikra mbalimbali na zaidi zile za ajabu ajabu na zile zenye kupelekea kwenye maovu. Kuna ambao huitumia faragha katika kumkumbuka Allaah na kukumbuka mauti na kukumbuka maumbile na utukufu wa Allaah, lakini kuna wengi hutumia faragha kuyafikiria maasi, maovu na hata kuyaendea.

 

Tumia muda wako wa faragha kujighulisha na ya kheri; kusoma Qur-aan,, Adhkaar, vitabu vya Dini, kusikiliza Qur-aan, mawaidha, kutazama video za Dini n.k. Hiyo itakusaidia sana na kuingiliwa na fikra za kufru na Ibiliys kupata upenyo wa kukuchezea.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

Wasiwasi Wa Shaytwaan Unamfanya Afikirie Mambo Ya Kufru, Afanyeje?

Imani Yangu Inapungua Nakhofu Kupotoka Nifanyeje?

 

Allaah Anajua zaidi

 

Share