Kusoma Nyiradi Kwa Sauti Kwa Ajili Ya Kuwafunza Watoto

SWALI:

 

Assalam aleikum warahmatullahi wabarakatu. ama baada. kwanza ningependa kutoa shukrani kwa wote wale wanaohusika na mtandao huu.ni mengi ya faida tumejifuza hapa na mengi yametutoa ujingani. Shukrani zote kwa Allah nanyie atawajazi kheri.

 

Swala langu ni masala ya kuomba mungu kwa sauti ya juu. Nimepitia aya 205 katika suratul A'araf inayo eleza kuhusu haya. Ningependa munitowe tashwishi mbili juu ya haya 1. Nina watoto nyumbani na napenda nyuradi ninazo soma asubuhi na jioni na wao wkamatane nazo ili wainukie wakijua namna ya kumuoba Allah Subhana Wataala. Itanibidi nisome kwa sauti ya juu ili wanisikie vipi hukmu yake?


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu ufahamu wa Aayah hiyo uliyoitaja hapo juu.

Mwanzo tunatakiwa tufahamu kuwa tunatakiwa tufahamu kuwa kuna tofauti baina ya nyiradi na du’aa mbali na kuwa du’aa nyingine ni nyiradi. Du’aa kama ilivyokuja katika Aayah ni suala linalofungamana baina ya mja na Muumba wake kwa yale anayotaka mja.

Ama katika kutaka watoto waweze kushika hizo nyiradi ambazo zimesuniwa katika shari’ah basi hakuna tatizo kunyanyua sauti ili watoto waweze kushika na kuhifadhi ili wainukie katika hali hiyo. Na hilo litakuwa ni jambo jema kwako na kwao.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share