Maana Ya Mchumba Kishari’ah

SWALI:

 

Assalaam alaikum, Ndugu zangu katika uislam napenda kujua nini maana ya mchumba katika sheria ya kiislam, kwani mtu akiwa amekubaliana na mwanamke kumuoa lakini hajenda kwao rasmin kwa ajili ya kumposa huyo binti waliokubaliana ila mwanamke tayari ameshawambia jamaa zake wote kua wamekubaliana na mtu fulani kuoana yaani baba, mama, kaka shangazi n.k na wote hao jamaa wamekubali hayo waloelezwa na binti yao na huyo mwanamme anajulikana upande wa huyo mwanamke je huyu ataitwa mchumba na kama si mchumba ataitwaje katika sheria ya kiislam maasalaam.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu maana ya uchumba katika Uislamu.

 Uchumba katika Uislamu ni pale mwanamme anayetaka kuoa au jamaa zake au mtu yeyote aliyemwakilisha anapokwenda kwa wazazi wa msichana kuposa na kukubaliwa.

Huo ndio unaitwa uchumba kinyume na hivyo unakuwa ni urafiki baina ya mvulana na msichana. Na hili limekatazwa kishari’ah.

 

Na hata baada ya mvulana kupeleka posa rasmi kwa wazazi wa msichana, hao wawili hawajaruhusiwa kishari’ah kutembea pamoja, kukutana au hata kuwasiliana bila ya dharura.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share