054-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Kujikinga Kutokana Na Mambo Manne Kabla Ya Kuomba Du’aa

 

Wajibu Wa Kujikinga Kutokana Na Mambo Manne Kabla Ya Kuomba Du’aa

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakapomaliza mmoja wenu Tashahhud (ya mwisho) aombe kujikinga kwa Allaah kutokana na mambo manne, aseme:

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ جَهَـنَّم، وَمِـنْ عَذابِ القَـبْرِ، وَمِـنْ فِتْـنَةِ  المْحْـيا وَالمْمـاتِ، وَمِـنْ شَـرِّ (فِتْـنَةِ)  المْْسِيحِ الدَّجَّال

 

“Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min ‘adhaabi Jahannam, wamin ‘adhaabil qabri, wa min fitnatil mahyaa wal-mamaat, wamin sharri [fitnatil] Masiyhid-Dajjaal”

 

“Ee Allaah, mimi najikinga Kwako] na adhabu za  moto (wa Jahannam) na adhabu za kaburi na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya [fitna] ya Masiyhid-Dajjaal)) [Kisha ajiombee mwenyewe kinachompata]([1]) Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiomba (du’aa) katika Tashahhud yake”([2])

 

Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwafundisha Maswahaba (رضي الله عنهم) hivyo kama alivyowafundisha Surah za Qur-aan”([3])

 

 [1] Muslim, Abu ‘Awaanah, An-Nasaaiy na Ibn Al-Jaruud katika Al-Muntaqaa (27). Imetolewa katika Al-Irwaa (350).

[2] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[3]  Muslim na Abu ‘Awaanah.

Share