056-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Tasliym (Kutoka Salaam) Na Uwajibu Wake

 

 

Tasliym (Kutoka Salaam)

 

Kisha, “Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa salaam upande wa kulia:

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ

 

Assalaamu ‘Alaykum wa  RahmatuLlaah

 

“Amani na Rahma iwe juu yenu” (akigeuka hadi weupe wa shavu lake la kulia ukionekana)

 

Na upande wa kushoto:

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ

 

Assalaamu ‘Alaykum wa  RahmatuLlaah

 

“Amani na Rahma iwe juu yenu”

 

 (akigeuka hadi weupe wa shavu lake la kushoto ukionekana)”([1])  Mara nyingine aliongeza katika maamkizi upande wa kulia:

وَبَرَكَاتُهُ

Wa Barakaatuh

 

…Na Baraka Zake (zishuke kwenu)([2])

 

"Aliposema

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ

 

Assalaamu ‘Alaykum wa  RahmatuLlaahi

“Amani na Rahma ya Allaah iwe juu yenu”

Upande wa kulia, alipunguza mara nyingine alipatoa salamu upande wa kushoto;

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ

 

Assalaamu ‘Alaykum

“Amani iwe juu yenu”([3])

 

Mara nyingine, "aliamkia mara moja tu:

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ

Assalaamu ‘Alaykum 

 

Amani iwe juu yenu”

(mbele ya uso wake akigeuza upande wake wa kulia kidogo) [au kidogo tu]"([4])

"Walikuwa wakiashiria mikono yao walipotoa slaamu upande wa kulia na kushoto; Alipowaona Mjumbe wa Allaah   (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ((Mna nini nyinyi? Mnaashiria mikono yenu kama kwamba ni mikia ya farasi mwitu?! Anapotoa salamu mmoja wenu, atazame mbele ya mwenziwe na sio kuashiria kwa mikono yake))

 

Hivyo waliposwali naye, hawakuashiria) [katika riwaaya nyingine: ((Inatosheleza kila mmoja wenu kuweka mkono wake pajani kisha kutoa slaamu kwa nduguye aliyoko upande wa kulia kwake au kushoto))([5])

 

 

 

Wajibu Wa Tasliym (Kutoa Salaam)

 

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((…na inamalizika (yaani Swalah) kwa tasliym))([6])

 

 

 

 

[1] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh.

[2] Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah (1/82/2) ikiwa na isnaad Swahiyh.

‘Abdul-Haqq pia amekiri kuwa ni Swahiyh katika Ahkaam (56/2) kama alivyokiri An-Nawawiy na Ibn Hajar. Pia imesimuliwa kupitia njia nyingine na ‘Abdur-Razzaaq katika Muswannaf (2/219). Abu Ya’ala katika Musnad yake (3/1253), At-Twabaraaniy katika Mu’jam Al-Kabiyr (3/67/2) na Mu’jam Al-Awswatw (Namba: 4476 – Nambari zangu) na Ad-Daaraqutwniy.

[3] An-Nasaaiy, Ahmad na Siraaj ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4] Ibn Khuzaymah, Al-Bayhaqiy, Adh-Dhwiyaa katika Al-Mukhtaarah na 'Abdul-Ghaaniy Al-Maqdisiy katika Sunan yake (243/1) ikiwa na isnaad Swahiyh; Ahmad, At-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Awswatw (32/2), Al-Bayhaqi, Ibn Al-Mulaqqin (29/1) na Al-Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Takhriyj yake imetolewa katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl katika Hadiyth Namba 327.

[5] Muslim, Abu 'Awaanah, Siraaj, Ibn Khuzaymah na At-Twabaraaniy.

 

 

TANBIHI:

 

Maibaadhi wamegeuza Hadiyth hii. ‘Aalim wao Rabiy' amesimulia katika Musnad isiyotegemewa ikiwa na kauli mbali mbali kuthibitisha rai zao kwamba kunyanyua mikono pamoja na takbiyr inatengua Swalah! Kauli hiyo ni uongo, kama nilivyoelezea katika Adh-Dhwa'iyfah (6044).

[6] Al-Al-Haakim, na Adh-Dhahabiy amekiri Swahiyh. Imeshatolewa kikamilifu katika 'Takbiyr' ya kufungulia.

 

Share