Mashaytwaan Wanaweza Kusababisha Kubadilisha Vipimo Vya Damu?

SWALI:

 

Assalam Aleykum.

Mimi napeda kupata ufafanuzi wa juu ya swali lifuatalo.

Je Mashetani yanapokuwa ndani ya mwili wa binadamu yanaweza kusababisha vipimo (vya hospital) kama vya kifua, choo au damu (yaani vipimo vionyeshe kuwa mtu ana ukimwi wakati hana? Na pia kumsababishia mtoto kuwa mgonjwa mara kwa mara?

Alhamdulilah, Nitazidi kushukuru sana kwa majibu yatakayo tolewa pamoja na ushauri wa nini cha kufanya endapo upo kwenye Mtihani huo.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu uwezo wa mashaytwaan katika mwili wa mwanaadamu.

Hakika ni kuwa kwa uwezo aliopatiwa shaytwaan na Allaah Aliyetukuka ni kuwa shaytwaan anaweza kufanya hivyo kwa kubadilisha yaliyomo ndani ya mwanaadamu.

Hata hivyo, shaytwaan hawezi kubadilisha chochote au kuleta athari yoyote katika mwili wa mwanaadamu ila kwa idhini yake Allaah Aliyetukuka.

 

Kwa minajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Anatuelezea:

Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Allaah. Na wanajifunza yatayowadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walichojiuzia nafsi zao laiti wangelijua” (al-Baqarah 2: 102).

 

Ikiwa mtu amesibiwa na shaytwaan itabidi apatiwe kinga kwa kusomewa na Muislamu mwenye Imani na ujuzi wa kisomo cha Ruqyah ili atolewe ndani ya mwili. Na baada ya hapo inabidi mtu mwenyewe awe atajilinda kwa kusoma Aayah, Surah na adhkaar ambazo zitampatia kinga hiyo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share