Shemeji Aliyefariki Anamjia Ndotoni Kuwa Kuna Mtu Anamfanyia Uchawi- Je Aende Kwa Maalim Atolewe Uchawi?

 

Shemeji Aliyefariki Anamjia Ndotoni Kuwa Kuna Mtu Anamfanyia

Uchawi- Je Aende Kwa Maalim Atolewe Uchawi?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Assalam Ayaykum warahmatullahi wabarakat.

 

Suala langu kuwa kuna shemeji yangu amekufa ghafla lakini kila mara namuona na mara ya mwisho amekuja usiku baada ya saa sita akaniambia kuwa katumwa na mtu ambaye namjua kuja kuniingiza uchawini lakini kwa uwezo wake Subhaanahu wa Ta'aalaa nikapata nguvu ya kumtupia mto ambao nilikuwa nimeulalia akapotea na kila niamkapo asubuhi lazima naona masinzi kwenye shuka na kila ninapo lala nasoma dua na yaseen kamili na kucha naeka cassette ya Qu-raan lakini bado mambo yananifuata mwisho nimeamua nataka kwenda kwa maalim lakini naogopa dhambi je nifanye nini? mimi naishi Oman sasa miaka 20 na umri wangu miaka 33 naomba msaada kutoka kewnu.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Asli katika kifo ni kuja ghafla na hilo halina wa kulizuilia wala halifungamani na kitu chochote au sababu yoyote ile, ndio kifo kilivyowekwa kuja. Kujiwa usingizini na mtu aliyekufa ni miongoni mwa mambo yanayotokea na kauli yako kuwa amekuambia kuwa ametumwa hiyo inathibbitisha kuwa ni Shaytwaan; kwani aliyekufa hana njia ya kuja unaweza kumuota kama waliojaaliwa humuota Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na usemi wako kuwa katumwa na mtu ambaye namjua kuja kuniingiza uchawini unathibitisha kuwa huyo ni katika mashaytwaan kwani wao ndio wenye kusukuma na kupendezea watu uchawi ambao ni kufru na shirk.

 

Unachotakiwa kufanya ni kila unapokwenda kulala kuleta dhikr zilizothibiti zikiwemo kusoma Qul Huwa Allaahu Ahad, Qul A'udhu birabbil Falaq na Qul A'udhu birabbin Naas, Aayatul Kursiy na nyiradi nyingine zilizopokelewa  Ingia katika kiungo kifautacho usome nyiradi ambazo ni kinga kubwa kwa Muislamu kutokana na kila shari. Fululiza kuzisoma hizi na Insha Allaah kwa utapata hifadhi ya Allaah:

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

 

028-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Kulala

 

 

Pia soma maswali na majibu katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Je Uchawi Upo? Na Vipi Kujitibu?

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Inafaa Kwenda Kwa Waganga Kujitibu Uchawi?

 

Kujikinga Na Ushirikina Wa Uchawi Na Mauaji

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

Aayatul Kursiy ni miongoni mwa Aayah zilizopokelewa kuwa zikisomwa mtu huwa chini ya hifadhi yake al-Haafidh na sio Yaasiyn wala kuacha kucha cassette ya Qur-aan, Qur-aan unatakiwa uisome wewe au uisikilize ikiwa inasomwa, sio kuacha cassete ya Qur-aan bila ya kuwepo msikilizaji hilo halijapokewa katika yaliyopokewa yenye kuhusiana na Qur-aan kuisoma au kuisikiliza.

 

Ama uamuzi wako wa kutaka kwenda kwa maalim lakini unaogopa dhambi na hujuwi ufanye nini, hili linashangaza kwani la kufanya unalo, shikamana na Qur-aan utafanikiwa, shikamana na mafundisho ya dini utahifadhiwa, mhifadhi Allaah Atakuhifadhi.

 

Huyu unayemuita maalim huyo ni Kaahin-mpiga bao- na ni Dajjaal, ni mtihani na fitna kwako katika Dini yako; kwani yeye hujidai kutoa habari za ghayb katika mambo yajayo na wenye kumuendea kaahin Maulamaa wamewagawa makundi matatu:

 

1.     Mwenye kwenda kwa kuhaan (mpiga ramli) na kumuuliza pasina kumsadiki na kuwafiki atayoyasema , kwani yote ayasemayo huwa ni uwongo mtupu, hali hii ni haramu kulifanya na mfanyaji ambaye amekwenda kwa mpiga bao, adhabu yake Swaalah zake za siku arubaini 40 huwa hazikubaliwi kama ilivyothibi katika Sunnah kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Mwenye kumuendea mpiga bao na kumuuliza tu, Swaalah zake za siku arubaini huwa hazikubaliwi, au masiku arubaini" Imepokelewa na Muslim, kitabul cha as Slaam, mlango uharamu wa al Kah-nah na kwenda kwa Makuhaani.

 

2.     Mwenye kwenda kwa kuhhaan akamuuliza kisha akasadikisha na akamuwafiki katika anayoyazua, kwani yote ayasemayo huwa ni uwongo mtupu, hali hii ni huwa kufr mtu huwa keshakufuru, kwani huwa amemkubalia katika madai yake kuwa anaelewa mambo ya ghayb; na kumkubalia au kumsadikisha kiumbe katika madai yake kuwa anaelewa mambo ya ghayb ni kuikana na kuikata waziwazi kauli yake Allaah:

 

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa. [An-Naml: 65].

 

Pia humtoa mto katika dini jambo ambalo ni hatari kubwa kwa Muislamu:

 

"Atakayemwendea mchawi na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad [Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam" [Abu Daawuud]

 

3.     Mwenye kwenda kwa kuhhaan na kumuuliza kwa lengo la kutaka watu wamuelewa na kumbaini uwongo wake na kuwa yeye ni kuhhaan na hana alijuwalo isipokuwa ni mfitinishaji na ni mzushi na mtoposhaji, hali hii haina tatizo insha Allaah.

 

Kutokana na hayo, tunakupa nasaha ujiepushe na hayo na ufuate mafunzo ya dini yako Swahiyh na Allaah Atakuhifadhi kwa kila shari Insha Allaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share