Mume Ana Hiari Kukaa Kwenye Mtandao Masaa Kila Siku, Lakini Inapita Miezi Na Hamtimizii Mkewe Haki Ya Tendo La Ndoa

SWALI:

 

assalam  aleykum .kwanza kabisa  ningependa kuwashukuruni.

suwala  ni kama  lifuatavyo mimi nimeolewa  lakini mume wangu hana  time

na  mimi hata  kwenye tendo la ndoa  tunafika  kukaa mpaka  miezi mitatu au zaid bila ya kuingiliana  na  yeye  anatumia usiku  mwingi kwenye internet   na  mimi nishamwambia sipendo mwendo wake huo  lakini jibu lake ni  kuwa yeye  hawezi kuishi bila ya internet anaweza kuishi bila ya mimi lakini sio  bila ya internet kwa hiyo mimi mwenyewe najiona  mimi kwake yeye sina thamani kuliko ya hiyo internet  je ndoa hii  inakubalika  shekhe? 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mume kuthamini mtandao (internet) kuliko wewe.

Hakika hili ni tatizo sugu katika jamii yetu na huenda mtu akajiuliza ikiwa mume anathamini kitu kingine chochote kuliko mke ingekuwa bora kwake kutoingia katika ndoa.

 

Mambo ambayo unaweza kufanya ni kama yafuatayo:

 

  1. Ni wewe kutafuta wakati munasibu kuweza kuzungumza na mumeo kwa mara nyengine tena kwa hekima, ulaini, upole na mawaidha mazuri kuhusu mahusiano yenu ya uwanandoa.

 

  1. Huenda mumeo hajui majukumu na wajibu wake katika ndoa. Kwa minajili hiyo itabidi utafute vitabu na kaseti inayozungumzia unyumba. Huenda kupata hayo akabadilika.

 

  1. Itisha kikao baina yako wewe, mumeo na wawakilishi wako na wa mumeo. Wawakilishi wenu wanaweza kuwa wazazi au jamaa za karibu. Na katika kikao hicho uzungumze wazi kwa yanajiri na kutokea. Kufanya hivyo huenda ikatoa ufumbuzi mzuri.

 

  1. Ikiwa hakujirekebisha itabidi uende kwa Qaadhi ili umshitakie hilo. Na ikiwa ataona kuwa mtandao (internet) bado ni bora kuliko wewe basi itabidi muachane ili usiwe ni mwenye kudhulumiwa.

 Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Mume Anakesha Katika Internet Hampi Mke Haki Yake - Mke Afanyeje?

Twamuomba Allaah Aliyetukuka Akutoe ufumbuzi wa shida hiyo na muweze kuishi na mumeo kwa njia iliyo nzuri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share