Sindano ya Ganzi na Kung'oa Jino Inavunja Swawm?

SWALI:

Assalam alykum

Naomba mnifahamishe kuhusu  shindnao ya gazi.

 Ikiwa mtu kapigwa shindano ya gazi anapotolewa jino, na alikua kafunga sasa aendelee na kufunga au itambidi alipe funga yake

Assalam Alyku.JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunaomba samahani kuchelewa kukujibu kwani swali lako bila shaka lilihitajia kujibiwa haraka kutokana na hali yako hiyo.

Jibu ni kwamba unapoomuwa na jino na inapobidi ung'olewe basi huna budi kufanya hivyo ili usitaabike zaidi na maumivu. Na kupiga sindano ya ganzi haina tatizo na Swawm yako. Kwa hiyo unaweza kupiga sindano ya ganzi na kutolewa jino na Swawm yako itabaki kuwa sahihi. Tahadhari tu usimeze damu au dawa ya kusukutua ikasababisha kuharibu Swawm yako.

 

Na Allah Anajua zaidi

 

Share