Kujipaka Vipodozi Wakati Wa Swawm

SWALI:

 

assalam aleikum kwanza ningependa kutoa shukrani nyingi sana kwa alhidaya kwa kutuwezesha sisi waislam kuelewa vizuri dini yetu asante saaana pili nina swali kwa sisi wanawake je kupaka rangi ya mdomo kwa aliefunga swaum ni sawa katika dini yetu tukufu je imeruhusiwa?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Aina yoyote ya madawa au vipodozi ambavyo vinapakwa nje ya mwili ikiwa kwa ajili ya matibabu au kulainisha ngozi n.k. haibatilishi Swawm wala haihitaji kulipwa.

 

Lakini mwanamke kujiremba akatoka nje na kuonekana na wasio Maharimu wake ni jambo lisliopasa kufanywa kwani ni kuonyesha mapambo yake ambayo ameamrishwa kuyaficha. Amri hii inampasa aitekeleze siku zote na sio tu katika mwezi wa Ramadhaan pekee.

 

Kwa hiyo mwanamke ajiepushe na kila aina ya mapambo ili asisababishe fitna ya kutamaniwa na wanaume, khaswa mwezi huu unapaswa kupewa heshima yake zaidi na kuzingatiwa ili ibada ya Swawm na nyinginezo zote zibakie katika usalama bila ya upungufu wa thawabu na kuchuma dhambi.

 

  

Na Allaah Anajua zaidi

   

 

Share