12-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Hitimisho

 

12- Shaykh Al-Islaam Ibn Tamiyyah: Hitimisho

 

Alhidaaya.com

 

 

Hitimisho

 

Miongoni mwa wachache, ambao dunia imewapata, kama ni mtu mwenye ubongo wenye kufahamu sana, hadhi na sifa, Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah alikuwa ni mmoja wao. Sifa zake bora na hadhi yake pekee kama ni Mwanachuoni wa Kiislamu ni zaidi ya utangulizi wowote. Wanachuoni wengi wakubwa kwa wakati wetu wanaonekana kuwa ni wenye kuikusanya elimu yake. Amechangia mengi taqriban katika misingi na matawi yote na vitovu vya elimu ya Kiislamu.

 

Mawazo yake, fikra na maamuzi yameathiri kwa mapana nyanja tofauti za maisha ya Kiislamu.

 

Shaykh al-Islaam alikuwa ni mwenye kuzikamata vyema dhana na imani za madhehebu tofauti ya Kiislamu na halikadhalika Ukiristo. Ndani ya kazi zake, amechukua ilani makini katika imani zote hizi na kunyofoa kutokana nazo Imani sahihi na bora na kuufundisha Uislamu.

 

Ibn Taymiyyah amejenga mazingira ya kimapinduzi ya kifikra kupitia mapote yote mawili; fikra zake na jitihada zake za uhuishaji ambayo athari yake zinahisiwa si tu kwa wakati wake lakini tokea enzi hizo hadi leo. Katika wakati wake, watu walikuwa wamegawika aidha katika wale ambao walikuwa ni wapinzani wenye nguvu au wafuasi wenye nguvu ambao kwa ukamilifu wamemkubali, au wasiojikubalisha, ambao walikubali baadhi ya mawazo na kukataa baadhi. Ibn Taymiyyah ameacha nyuma idadi kubwa kabisa ya vitabu na ustaarabu. Wapinzani wake ghafla wakazama kwenye kutojulikana, hali ya kuwa hadhi na kukubalika kwa kazi zake kumeongezeka.

 

Katika maisha yake, umaarufu wa Ibn Taymiyyah na taathira zake, ulienea zaidi ya mipaka ya Misri na Syria. Alipofungwa kwa mara ya mwisho ndani ya jela ya Damascus, barua nyingi zilikuja kutoka kwa wakaazi wa Baghdad wakipinga kukamatwa kwake na kutaka aachiwe huru. Alipokufa, Swalah ya maziko ilifanyika katika kila ardhi waliosikia kifo chake.

 

Ilikuwa ni muhimu kuandika kuhusiana na mtu huyu mkubwa; Mwanachuoni mkubwa aliyeishi baada ya vizazi vitatu bora, kizazi cha warithi wa waongofu (Salaf as-Swaalih).

 

 

 

Share