Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

 

 

Vipimo Vya Wali

Mchele Basmati - 4 vikombe

Vitunguu vya majani (Spring onions) - 5 miche

Pilipili mboga nyekundu (capsicum) - 1

Pilipili mboga manjano (capscimu) - 1

Nyanya kubwa - 1

Supu ya kidonge - 2

Siagi - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha mchele kisha roweka kiasi masaa matatu takriban.
  2. Katakata vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya vipande kiasi.
  3. Weka siagi katika sufuria ya kupikia, weka katika moto iyayuke.
  4. Tia vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya, kaanga kidogo tu.
  5. Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji kiasi ya kuivisha mchele.
  6. Tia supu ya kidogo au supu yoyote, funika wali upikike moto. mdogodogo.

Vipimo Vya Nyama Mbuzi Na Sosi Ya Ukwaju

Nyama mbuzi mapande makubwa kiasi - 7/8 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Ukwaju mzito ulokamuliwa - 1 kikombe cha chai

Jiyra/cummin/bizari pilau - 1 kijiko cha chai

Nyanya kopo - 2 vijiko vya supu

Siki - 2 vijiko vya supu

Mafuta - ½ kikombe cha chai

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya vitu vyote pamoja katika kibakuli kidogo.
  2. Weka nyama katika bakuli kubwa kisha tia mchanganyiko wa sosi, ubakishe sosi  kiasi pembeni.
  3. Roweka kwa muda wa masaa 3 – 5
  4. Panga nyama katika bakuli au treya ya kuchomea   katika oven.
  5. Pika (bake)  kwa moto wa kiasi kwa muda wa saa takriban.
  6. Karibu na kuiva, epua, zidisha kuichangaya na sosi ilobaki.
  7. Rudisha katika jiko uendelee kuipika muda kidogo tu.
  8. Epua ikiwa tayari, weka juu ya wali uliopakuwa kisha mwagia sosi ya nyanya pilipili  (chilii tomato sauce) ukipenda.

 

Share