056-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Masikini Amtazame Aliye Chini Yake Wala Asitazame Aliye Juu Yake

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 56

Masikini Amtazame Aliye Chini Yake Wala Asitazame Aliye Juu Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْكُمْ وَلاَ تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ فَإِنَّهُ أَجْدَرُ أَنْ لاَ تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ)) متفق عليه وهذا لفظ مسلم.

 وفي رواية البخاري: ((إِذَا نَظَرَ أَحَدُكُمْ إِلَى مَنْ فُضِّلَ عَلَيْهِ فِي الْمَالِ وَالْخَلْقِ فَلْيَنْظُرْ إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mtazameni aliye chini yenu wala msimtazame aliye juu yenu, kwani [kufanya hivyo] ni haki zaidi msije  mkazidharau neema za Allaah juu yenu))[ Al-Bukhaariy na Muslim] Hii ni lafdhi ya Muslim.

 

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: ((Anapomtazama mmoja wenu aliyefadhilishwa zaidi kwa mali na umbo, basi amtazame aliye chini yake)).

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Hikma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kujaaliwa baadhi ya watu matajiri, na baadhi yao masikini na kuwafadhalisha wengine juu ya wengineo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾

Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia juhudi inayostahiki kufanyiwa, naye ni Muumin, basi hao juhudi zao ni za kushukuriwa. 

كُلًّا نُّمِدُّ هَـٰؤُلَاءِ وَهَـٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا ﴿٢٠﴾

Wote hao Tunawakunjulia; hawa na hao katika hiba za Rabb wako. Na hazikuwa hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa.

انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا ﴿٢١﴾

Tazama vipi Tunavyowafadhilisha baadhi yao juu ya wengineo. Na bila shaka Aakhirah ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi. [Al-Israa 17: 19-21)]

 

 

2. Ni bora kumtazama aliye chini katika mambo ya mali duniani. Ama mas-alah ya Dini, ni jambo zuri kumtazama aliye juu ili Muislamu apate kujihimiza na kushindana kutenda ‘amali au kujifunza na amfikie nduguye huyo.  Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

Na kheri yoyote waifanyayo hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni Mjuzi wa wenye taqwa.  [Aal-‘Imraan (3: 113-115)]

 

Rejea pia: Al-Muttwaffifiyn (83: 26), Al-Muuminuwn (23: 60-61).

 

 

3. Kumtazama aliye chini husaidia kukumbuka neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na kushukuru kwa majaaliwa.

 

 

4. Haitakiwi kutamani kwa wivu na husda neema alizojaaliwa mwengine, bali ni kumshukuru na kumwomba Allaah (سبحانه وتعالى). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚوَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾

Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [An-Nisaa (4: 32)]

 

Rejea pia: An-Nahl (16: 71).

 

 

5. Kumtazama aliye juu hupelekea kukufuru neema za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

 

 

 

 

 

 

Share