112-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ikhtilaatw - Wanawake Kuchanganyika Na Wasio Mahaarim

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 112

 

Ikhtilaatw – Wanawake Kuchanganyika Na Wasio Mahaarim

 

 

 

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِيَّاكُمْ وَالدُّخُولَ عَلَى النِّسَاءِ)) فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ الأَنْصَارِ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَفَرَأَيْتَ الْحَمْوَ؟ قَالَ:  ((الْحَمْوُ الْمَوْتُ))  متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Tahadharini na kuingia kwa wanawake!)) Mtu mmoja katika Answaariy akauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Nieleze akiwa ni shemeji?” Akamwambia:  ((Shemeji ni mauti!)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Mahaarim au Mahram ni wanaume ambao hawaruhusiki ki-shariy’ah kuwaoa wanawake kama vile baba, ‘ammi, mjomba, kaka, watoto wa dada na watoto wa kaka.

 

 

2. Al-Hamw ni jamaa wa karibu wa mume kama kaka yake, mtoto wa kaka yake, mtoto wa ‘ami yake n.k.

 

 

3. Makatazo ya ikhtilaatw (kuchanganyikbaina ya wanaume na wanawake wasio mahaarim zao kama Alivyokataza Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ ۚ

Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao [Al-Ahzaab (33: 53)]

 

 

4. Makatazo ya jamaa za mume kuwa faragha na mke, kwani hilo ni jepesi kuchanganyika nao, kwa vile wako karibu na kutokea fitna ni wepesi kabisa.

Hadiyth: Kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hachanganyiki mwanamume na mwanamke ila shaytwaan huwa ni watatu wao)). [At-Tirmidhiy]

 

 

5. Uislamu umetahadharisha kila aina ya shari na kukaribia zinaa na umehimiza amani baina ya jamii. 

 

Rejea: Al-Israa (17: 32).

 

 

6. Kufananishwa Al-Hamw na mauti ni dalili jinsi uwezekano mwepesi wa kutokea fitna, kwani aghlabu shemeji huwa na huruma.

 

 

7. Tatizo kubwa lipo katika jamii kuchanganyika na mashemeji, na ndio maana fitna nyingi hutokea katika jamii.

 

 

8. Ni kawaida kwa watu kutochukua tahadhari kwa maingiliano kama hayo na madhara yake ni makubwa katika jamii.

Share