113-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Wamelaaniwa Wanaume Wanaojifananisha Na Wanawake Na Wanawake Wanaojifananisha Na Wanaume

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 113

 

Wamelaaniwa Wanaume Wanaojifananisha Na Wanawake

Na Wanawake Wanaojifananisha Na Wanaume

 

 

 

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: لَعَنَ رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُخَنَّثِينَ مِنْ الرِّجَالِ وَالْمُتَرَجّلاتِ مِنْ النِّسَاءِ. وفي رواية: لَعَنَ رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُتَشَبِّهِينَ مِنْ الرِّجَالِ بِالنِّسَاءِ وَالْمُتَشَبِّهَاتِ مِنْ النِّسَاءِ بِالرِّجَالِ. البخاري

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifananisha na wanaume”. Na katika riwaya nyingine imesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewalaani wanaume wanaojishabihisha na wanawake, na wanawake wanaojishabihisha na wanaume.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Haramisho la wanaume na wanawake kujifananisha sawa kwa mavazi, sauti, mwendo, mapambo n.k. kwani hivyo ni upotofu wa shaytwaan aliyeahidi kuwapotoa. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewatahadharisha kwa makazi ya moto kama Anavyosema:

 

 لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾

Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: “Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu.”

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

 “Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.” Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana.

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢٠﴾

Anawaahidi na anawashawishi matamanio ya uongo. Na shaytwaan hawaahidi isipokuwa ulaghai.

 

أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾

Hao makaazi yao ni Jahannam, na wala hawatopata makimbilio ya kutoka humo. [An-Nisaa (4: 118-121)]

 

 

2. Inapotajwa laana katika Aayah au Hadiyth, basi ni uthibitisho kuwa jambo lililotajwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, kwani laana ni kuwekwa mbali na Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

 

3. Wanaojifananisha na wengine, ni ukosefu wa adabu mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama kwamba kumkosoa kuwa umbo Alowaumba nalo la fitwrah (asili ya maumbile), limekosewa au halifai kwao, na hali Amemuumba mwana Aadam kwa kumtofautisha kiwiliwili, sura, rangi n.k. kwa hikmah Yake.

 

Rejea: Al-Muuminuwn (23: 12-14), At-Tiyn (95: 4), Ar-Ruwm (30: 22).

 

 

4. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameweka Shariy’ah za kumtosheleza bin Aadam zenye maslahi naye zitakazozuia ufisadi katika jamii. Rejea Al-Maaidah (5: 48).

 

 

Na pia mwendo mzuri kabisa wa kuigiza wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho [Al-Ahzaab (33: 21)]

 

 

5. Ufisadi umeenea katika jamii; wanaume kuiga mavazi na mapambo ya kike, kama kuweka nywele ndefu, kuvaa herini, kuvaa nguo za kubana n.k. Na wanawake kuvaa masuruwali ya kubana, kukata nywele fupi n.k. yote ambayo yanamtoa mtu kutoka katika fitwrah (umbile la asili aloumbwa nalo).

 

 

 

 

Share