18-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Kunyooka Katika Tawhiyd Ni Sababu Ya Kupata Husnul-Khaatimah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

18-Kunyooka Katika Tawhiyd Ni Sababu Ya Kupata Husnul-Khaatimah

 

 

 

Muislamu anapothibitika katika iymaan na taqwa, hubashiriwa Jannah wakati anapofikwa na mauti:  Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْتُوعَدُونَ﴿٣٠﴾

 

Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”

 

 

نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾

 

“Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.

 

نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾

“Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Fusw-Swilat: 30-32]

 

Kadhaalika, Muislamu anahitaji kuthibitika katika neno la Tawhiyd ili asalimike kaburini na aweze kujibu maswali matatu atakayoulizwa na Malaika wawili; Munkar na Nakiyr.

 

عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ))) البخاري  وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة

Imetoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha Illa-Allaah wa Anna Muhammadar-Rasuulu-Allaah" [Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.”)) [Ibraahiym: 27 - Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Neno hilo limepigiwa mfano na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni kama mti mzuri:

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَال: كُنَّا عِنْد رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ((أَخْبِرُونِي عَنْ شَجَرَة تُشْبِه - أَوْ - كَالرَّجُلِ الْمُسْلِم لاَ يَتَحَاتّ وَرَقهَا صَيْفًا وَلاَ شِتَاء وَتُؤْتِي أُكُلَهَا كُلّ حِين بِإِذْنِ رَبّهَا)) قَالَ اِبْن عُمَر: فَوَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة وَرَأَيْت أَبَا بَكْر وَعُمَر لاَ يَتَكَلَّمَانِ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّمَ فَلَمَّا لَمْ يَقُولُوا شَيْئًا. قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ: ((هِيَ النَّخْلَة)). فَلَمَّا قُمْنَا قُلْت لِعُمَرَ: يَا أَبَتَاهُ وَاَللَّه لَقَدْ كَانَ وَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة. قَالَ: مَا مَنَعَك أَنْ تَتَكَلَّم؟ قُلْت: لَمْ أَرَكُمْ تَتَكَلَّمُونَ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّم أَوْ أَقُول شَيْئًا.  قَالَ عُمَر: لَأَنْ تَكُون قُلْتهَا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ كَذَا وَكَذَا - البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: "Tulikuwa na Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi  wa sallam) akauliza: ((Niambieni kuhusu mti unaofanana na au kama Muislamu, ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto, wala wakati wa majira ya baridi, na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Rabb wake)). Ibn ‘Umar akasema: “Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona vibaya kujibu nilipoona Abuu Bakr na ‘Umar hawakujibu”. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Ni mtende)). Tulipoondoka, nilimwambia ‘Umar: “Ee baba yangu! Wa-Allaahi nilihisi kuwa ni mtende”. Akasema: “Kwa nini basi hukutaja?” Nikasema: “Nilikuoneni kimya, nikaona vibaya kusema kitu”. Akasema ‘Umar: "Ungelisema, ingelikuwa bora kwangu kuliko kadhaa na kadhaa” (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee). [Al-Bukhaariy]

 

 Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) imethibitisha hayo Anaposema:

 

 أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾

Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri kama mti mzuri mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni? (marefu mno).

 

 

تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾

Unatoa mazao yake kila wakati kwa idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.

 

 

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾

Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna imara.

 

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo.  [Ibraahiym: 24-27]

 

 

 

 

Share