23-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Anayethibitisha Tawhiyd Ataepushwa Na An-Naar (Moto) Siku ya Qiyaamah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

23-Anayethibitisha Tawhiyd Ataepushwa Na An-Naar (Moto) Siku ya Qiyaamah

 

 

 

 

Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ

((Hakuna mtu atakayekiri moyoni na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na An-Naar (Moto). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]

 

 

Akapokea tena tena Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  يَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ شَعِيرَةٍ مِنْ خَيْرٍ وَيَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ بُرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ وَيَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيْر .

((Atatoka Motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha uzani wa shairi. Na Atatoka Motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha mbegu moja. Na atatoka Motoni anayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha uzani wa punje). [Al-Bukhaariy (44) Muslim (193)]

 

Hadiyth ya ‘Ithbaan bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ

((Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar kwa anayesema: laa ilaaha illa Allaah akitafuta Wajihi wa Allaah)). [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)]

 

Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba:

 

سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ النَّارَ

Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayekiri moyoni na kushuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), basi Allaah Atamharamisha na An-Naar [Moto])). [Muslim (29)]

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah na Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba wameshuhudia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 ((إِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ. يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَأَنَا أَكْبَرُ. وَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا وَحْدِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَا شَرِيكَ لَهُ. قَالَ : صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا شَرِيكَ لِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ  قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، لِي الْمُلْكُ، وَلِيَ الْحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِي. ثم قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  مَنْ رُزِقَهُنَّ عِنْدَ مَوْتِهِ لَمْ تَمَسَّهُ النَّارُ))

((Mja akisema: “Laa ilaaha illa Allaah wa Allaahu Akbar.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa).  Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Nami ni Mkubwa.” Akisema mja: “Laa ilaaha illa Allaah Wahdahu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee). Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Pekee.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu laa shariyka Lahu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hana mshirika) Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi sina mshirika.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaah, Lahul-Mulku walahul-Hamdu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ufalme na Himdi ni Zake). Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, Ufalme na Himdi ni Zangu.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaah, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah) Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwangu.” Kisha Rasuli wa Allaah akasema: Atakayeruzukiwa [kauli] hiyo wakati wa mauti yake, An-Naar [Moto] haitomgusa)). [Ibn Maajah (3794) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (713).

 

 

Share