081 - At-Takwiyr

 

التَّكْوِير

 

081-At-Takwiyr

 

 

081-At-Takwiyr: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾

1. Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.[1]

 

 

 

وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na nyota zitakapoanguka, kupuputika na kutawanyika. 

 

 

 

وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na milima itakapoendeshwa iondoke ilipo.

 

 

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾

 

4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapotelekezwa.

 

 

 

وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾

5. Na wanyama mwitu watakapokusanywa.

 

 

وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾

6. Na bahari zitakapojazwa na kuwashwa moto.

 

 

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾

7. Na nafsi zitakapounganishwa na roho kisha kwa aina zake (wema kwa wema, waovu kwa waovu). [2]

 

 

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾

8. Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa yuhai atakapoulizwa.[3]

 

 

 

بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾

9. Kwa dhambi gani aliuliwa?

 

 

 

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾

10. Na sahifa za kurekodi (amali) zitakapotandazwa (na kukunjuliwa).[4]

 

 

 

 

وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾

11. Na mbingu zitakapobanduliwa.

 

 

وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾

12. Na moto uwakao vikali mno utakapowashwa.

 

 

وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾

13. Na Jannah itakapoletwa karibu.

 

 

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾

14. Nafsi itajua hapo yale iliyoyahudhurisha.[5]

 

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾

15. Basi Naapa kwa sayari zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku).

 

 

 

 

الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾

16. Zinazotembea na kujificha.

 

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾

17. Na Naapa kwa usiku unapoingia. 

 

 

 

وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾

18. Na Naapa kwa asubuhi inapopambazuka.

 

 

 

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾

19. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl).[6]

 

 

 

 

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh.

 

 

 

مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾

21. Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni).

 

 

 

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾

22. Na hakuwa swahibu yenu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) majnuni.[7]

 

 

 

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾

23. Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana.

 

 

 

وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾

24. Naye si mzuiaji wa (kuelezea mambo ya) ghaibu.

 

 

 

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Na hii (Qur-aan) si kauli ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

 

 

 

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi mnakwenda wapi?

 

 

 

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾

27. Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.

 

 

 

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾

28. Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika haki)

 

 

 

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb wa walimwengu.[8]

 

 

 

[1] Baadhi Ya Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:

 

Suwrah hii At-Takwiyr (81), Al-Infitwaar (82) na Al-Inshiqaaq (84) zinaanza kutaja baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُ رَأْىُ عَيْنٍ فَلْيَقْرَأْ ‏ ‏ إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ‏ و ‏  ‏إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ  ‏ وَ ‏  إذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ ‏

“Anayependa atazame Siku ya Qiyaamah kana kwamba anaiona kwa macho yake, na asome:

 

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾

Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake. [At-Takwiyr (81:1)]

 

Na

إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾

Mbingu itakapopasuka. [Al-Infitwaar (82:1)]

 

Na

إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾

Mbingu itakaporaruka. [Al-Inshiqaaq (84:1)]

 

[At-Tirmidhy, Ahmad. Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3333)]

 

Na Hadiyth ifuatayo imethibiti kuhusu jua na mwezi kuvurugika na kupoteza mwanga wake:

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ الْمُخْتَارِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ الدَّانَاجُ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ مُكَوَّرَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jua na mwezi zitakunjwa (zitakoshwa mwangaza wake) Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy Kitabu cha Uanzishaji wa Uumbaji (65)]

 

[2] Watu Watakusanywa Vikundi Vikundi Kulingana Na Imaan Zao Na Matendo Yao Mema Na Ya Shari:

 

Siku ya Qiyaamah, watu wataunganishwa katika vikundi vikundi kulingana na imaan zao na amali zao; Waumini pamoja na Waumini na makafiri kwa makafiri, na watu wa kheri pamoja na watu wa kheri, na watu wa shari pamoja na watu wa shari na kadhaalika. Na Tafsiyr ni kama ifuatavyo:

 

Yaani: Watu wa kila tendo maalumu wataunganishwa pamoja; wema kwa wema, na waovu kwa waovu. Waumini wataunganishwa na mahurilayni (wanawake wa Jannah wenye macho mazuri kabisa), na makafiri wataunganishwa na mashaytwaan. Hivi ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah:

وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا ۖ

Na wataswagwa wale waliokufuru kuelekea Jahannam vikundi-vikundi. [Az-Zumar (39:71)]

 

Na pia:

وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ

Na wataongozwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah vikundi-vikundi. [Az-Zumar (39:73)]

 

Na pia:

احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾

 (Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu. [Asw-Swaaffaat (37:22)]

 

[Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Rejea pia Al-Waaqi’ah (56:7).

 

[3] Watoto Wakike Walikuwa Wakizikwa Wazima Zama Za Ujaahiliyyah:

 

Rejea An-Nahl (16:57) ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja sababu ya makafiri kuwazika watoto wa kike wanapozaliwa kutokana na kuona aibu wao kujaaliwa watoto wa kike, lakini wakimsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Malaika ni mabanati Wake!  Ametakasika Allaah na Ametukuka na wanayompachika nayo! Rejea pia Asw-Swaaffaat (37:149-153), Al-Israa (17:40) na Az-Zukhruf (43:15-19).

 

[4] Sahifa Za Kurekodiwa Amali:

 

Rejea Al-Israa (17:13-14) kwenye faida na rejea mbalimbali na maudhui zinazohusiana. Rejea pia Al-Infitwaar (82:11-12), Az-Zalzalah (99:4-8). Rejea pia Qaaf (50:18) kwenye faida kuhusu kuchunga ulimi kwa kuwa hata neno dogo vipi linarekodiwa.

 

[5]  Kila Nafsi Itatambua Amali Zake Ilizozitenda Duniani

 

Rejea Kauli nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) kama hizo katika Suwrah Aal-‘Imraan (3:30), Al-Kahf  (18:49), Al-Qiyaamah (75:13).

 

[6] Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha Kuwa Wahy (Qur-aan) Umeteremshwa na Jibriyl (عليه السّلام):

 

Allaah (سبحانه وتعالى)  Anathibitisha kuwa Qur-aan imehifadhiwa na mashaytwaan [na kwamba imeteremshwa na Jibriyl (عليه السّلام)] kama Anavyosema:

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾

Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl)

 

(Jibriyl) ambaye ameteremka nayo kutoka kwa Allaah kama Ananvosema katika Kauli Yake nyengine:

نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ﴿١٩٣﴾ عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿١٩٤﴾

Ameiteremsha Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu. Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji. [Ash-Shu’araa (26:193-194)]

 

[Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[7]  Uthibitisho Wa Allaah Juu Ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Aayah hii na zinazofuatia hadi (25), Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaradd washirikina wa Makkah na kuthibitisha yafuatayo:

 

i) Anawaradd washirikina wa Makkah wanaomsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kila sifa ovu kama kuwa yeye ni majununi, na kuisingizia Qur-aan kuwa imetungwa na kadhaalika.  Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa swala hili.

 

ii) Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Jibriyl katika umbo lake la asili lenye mbawa mia sita kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، عَنِ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ زِرٍّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى  قَالَ رَأَى جِبْرِيلَ - عَلَيْهِ السَّلاَمُ - لَهُ سِتُّمِائَةِ جَنَاحٍ

Amesimulia Ash-Shaybaan kutoka kwa Zirr, kutoka kwa ‘Abdullaah (رضي الله عنهم) kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾

Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona. [An-Najm: 53:11)]

 

Amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Jibriyl (عليه السّلام) akiwa na mbawa mia sita.” [Muslim]

 

Rejea An-Najm (53:1-14)

 

iii) Kwamba Qur-aan haikuteremshwa na  mashaytwaan. Rejea Aayah ya juu namba (19). Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) :

 

وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ ﴿٢١٠﴾ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٢١١﴾ إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ ﴿٢١٢﴾

Na wala hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na wala haipasi kwao na wala hawawezi. Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kuisikiliza. [Ash-Shu’araa (26:210-212)]

 

[8] Itikadi Potofu Ya Qadariyyah (Qadaria Au Kadaria) Na Radd   Kupinga Kwao Qadar Ya Allaah:

 

Kundi la Qadariyyah (Qadaria au Kadaria) ni wanaopinga nguzo ya sita ya imaan ya Kiislamu ambayo ni kuamini Qadar ya Allaah iwe jambo la kheri au la shari. Wao wanaitakidi kuwa ayafanyayo mtu katika matendo, si kwa khiyari yake.

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) ameelezea itikadi zao katika Fatwa ifuatayo:

 

Swali:  Je Qadaria ni akina nani, na zipi sifa zao?

 

Sheikh Allaah Akuhifadhi. Umetaja kuhusu kuiamini Qadar. Kuna kundi linaitwa Qadariyyah, tunatamani kufahamu madhehebu yao yanakusudia nini?

 

Jibu:  Al-Qadariyyah (Qadaria au Kadaria) ni watu wanaopinga Qadar, na hii ni katika unasibisho mbaya, kwa sababu ilivyozoeleka ni kwamba, kila asifikae na kitu fulani, basi hubeba sifa ya hiko kitu, lakini hawa wako kinyume chake, wanasifika na Qadar lakini wenyewe hawaiamini hiyo Qadar.

 

Mtu mwenye itikadi ya Qadariyyah huwa anadai kwamba mwanaadam anajitosheleza katika matendo yake, na kwamba Allaah Haingilii chochote kile. Na baadhi yao huwa wanachupa mipaka kabisa kwa kusema: “Hakika Allaah Hayajui matendo ya mja mpaka yatokee!”  Umefahamu?

 

Hawa kwa Ahlu-Sunnah wanawaita “Qadariyyah Majuwsiyyah.”  Wanawaita Wamajusi na wanasema: “Qadariyyah ni Majusi wa Ummah huu.”  Je, umefahamu kivipi hadi iwe hivyo?

 

Wamajusi wanasema: “Huu ulimwengu una waumbaji wawili nuru (mwanga) na giza. Pale penye shari muumbaji wake ni giza. Na pale penye kheri muumbaji wake ni nuru. Wakafanya ulimwengu na vilivyomo vina waumbaji wawili. Qadariyyah nao wako hivyo hivyo! (Wanasema):

 

“Matendo ya waja na kile kitokacho kwao, wao ndio wanajitegemea nacho, na kile Afanyacho Allaah hiko ni Chake.” Wakafanana na Wamajusi kwa itikadi hii, ndio wakaitwa Wamajusi wa Ummah huu.

 

Na juu ya maelezo haya kuna Hadiyth lakini ni dhaifu, isipokuwa Ahlu-Sunnah waliitumia kwenye hii laqabu. Je, umefahamu? [Liqaat Al-Baabb Al-Maftuwh (233)]

 

Imaam As-Sa’diy ametafsiri ifuatavyo:

 

Aayah hii na zinazofanana nyenginezo, zina radd kwa kundi la Qadari wanaokanusha Qadar ya Allaah na wale wanaokanusha khiari ya mwanaadam kama ilivyojadiliwa nyuma. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

 

 

 

 

Share