098 - Al-Bayyinah

 

  الْبَيِّنَة

 

098-Al-Bayyinah

 

098-Al-Bayyinah: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾

1. Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu[1] na washirikina wenye kujitenga na hali waliyonayo (ya kukufuru) mpaka iwafikie hoja bayana.

 

 

 

 

رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾

2.  Nayo ni Rasuli kutoka kwa Allaah anayewasomea Suhuf zenye kutakaswa.[2]

  

 

 

فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾

3. Ndani yake humo mna maandiko yaliyonyooka sawasawa.

 

 

 

 

وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾

4. Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.[3]

 

 

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

5. Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, wadumu humo. Hao ndio waovu kabisa wa viumbe.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾

7. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio wema kabisa wa viumbe.

 

 

 

جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًاۖ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾

8. Jazaa yao iko kwa Rabb wao. Nayo ni Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye. Hayo ni kwa yule anayemkhofu Rabb wake.

 

 

 

[1] Ahlul-Kitaab (Watu Wa Kitabu):

 

Watu wa Kitabu wanaokusudiwa katika Qur-aan ni Mayahudi na Manaswara. Wameitwa Watu wa Kitabu kwa sababu Allaah (عزّ وجلّ)  Aliwateremshia Vitabu viwili kwa wana wa Israaiyl. Wa  kwanza kati yao ni  Nabiy Muwasaa (عليه السّلام)  ambaye Ameteremshiwa Tawraat.  Na wa pili wao ni Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  ambaye ameteremshiwa Injiyl.   Wanaitwa: Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu) na Ahlul-Kitaabayni (Watu wa Vitabu Viwili). Nao wana hukumu zinazowahusu wao ghairi ya zinazowahusu washirikina wengine. Lakini wanakusanyika pamoja na makafiri wengine kwa jina la ukafiri na shirki. Hivyo wao ni makafiri na washirikina, kama vile waabudu masanamu, waabudu nyota, na sayari na makafiri wengineo wote waliokufuru. [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb - Ibn Baaz]

 

[2] Suhuf (Maandiko Matukufu) Na Tofauti Baina Yake Na Vitabu Vinginenvyo Vya Mbinguni:

 

Rejea Al-A’laa (87:18), An-Najm (53:36).

 

[3] Kugawanyika Ahlul-Kitaab (Mayahudi Na Manaswaara) Na Onyo Kwa Ummah Wa Kiislamu:

 

Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) inaelezea:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ تَفَرَّقَتِ الْيَهُودُ عَلَى إِحْدَى وَسَبْعِينَ أَوِ اثْنَتَيْنِ وَسَبْعِينَ فِرْقَةً وَالنَّصَارَى مِثْلَ ذَلِكَ وَتَفْتَرِقُ أُمَّتِي عَلَى ثَلاَثٍ وَسَبْعِينَ فِرْقَةً ‏" ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى حَدِيثُ أَبِي هُرَيْرَةَ حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja au sabini na mbili, na wakagawanyika Manaswara mfano wa hayo, na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu.” [At-Tirmidhiy]

 

Na rejea Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:103), (3:105), Al-An’aam (6:159), Ar-Ruwm (30:32), Ash-Shuwraa (42:14) kupata faida nyenginezo:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida nyenginezo:

 

105-Aayah Na Mafunzo: Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu.

 

 

 

Share