04-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Inabatilisha ‘Amali

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno

 

04- Shirki Inabatilisha ‘Amali

 

Alhidaaya.com

 

 

‘Amali za Muislamu bila ya kuwa na niyyah safi kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au ikhlaasw, huwa hazina thamani mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili zifuatazo:

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾

Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya   chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zinazotawanyika. [Al-Furqaan: 23]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾

Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” [Az-Zumar: 65]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]

 

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja katika Hadiyth Al-Qudsiy:

 

 

عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))    

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: ‘‘‘‘Mimi Ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.”  Yaani: hatopata ujira wowote kwa amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]

 

 

Mfano bayana wa kubatilika ‘amali za mtu kwa anayetoa swadaqah kwa riyaa ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

 Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.  [Al-Baqarah: 264]

 

 

Share