Kumuoa Mwanamke Mwenye Mimba

 

 

 

 

SWALI:

 

Mwanamke mwenye mimba unaruhusiwa kumuowa?

 


 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kuhusu mwanamke ambaye ana mimba huwezi kumuoa. mfano ni kuwa ikiwa mimba ni ya halali kwa kuwa ima ameachwa au mume amefariki. Mwanamke huyo atakuwa katika eda, eda ya kufiwa ni miezi minne na siku kumi na ya kuachwa ni miezi mitatu, lakini kwa wote wawili ikiwa ana mimba itakuwa mpaka azae. Baada ya kuzaa ikiwa mwanamke hajarudiwa na mumewe ataweza kuolewa baada ya eda. Na katika jambo hili Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataa mwanamme kutia mbegu zake juu ya mbegu za nduguye.

 

 

Na Allaah ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share