044-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 044: أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 44: Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu

 

 أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? 

 

Sababun-Nuzuwl: 

Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Aayah hii imeteremshwa kuhusu Mayahudi wa Madiynah. Alikuwa mtu miongoni mwao akimwambia mume wa mwanawe, jamaa zake na Waislamu ambao wamenyonya ziwa moja: “Thibitika katika Dini uliyo nayo na anayokuamrisha mtu huu -  yaani Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) - kwa sababu mambo yake ni ya haki.” Wakawa wanaamrisha watu kwa hayo lakini wao wenyewe hawatekelezi. [Asbaab Nuzuwl Al-Qur-aan – An-Naysaaburiy]

 

Ibn Jurayj amesema kuhusu Aayah: Je, mnaamrisha watu (watende) mema na mnajisahu nafsi zenu…” Ni kuhusu Ahlul-Ktaab na wanafiki. Walikuwa wakiamrisha watu kuswali na kufunga swawm. Lakini wao hawakuwa wakitekeleza waliyokuwa wakiamrisha wengine. Allaah Akawakumbusha tabia yao hii. Kwa hiyo yeyote anayeamrisha watu kutenda mema, basi na awe miongoni mwa wa mwanzo kutekeelza”.

 

Na pia Muhammad bin Is-haaq amesimulia kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu:  “na mnajisahu nafsi zenu…” ina maana mnasahau kutekeleze nyinyi wenyewe.

Na kuhusu: “na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini?”.

Nyinyi mnakataza watu wasikanushe Unabiy na  ahadi mliyoitaja iliyomo kwenu katika Tawraat na hali nyinyi wenyewe mmeisahau yaani: Mmesahau ahadi Niliyofungamana nanyi kwamba mtamkubali Rasuli Wangu. Mmevunja ahadi na mmekanusha mliyoyajua katika Kitabu Changu?  [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share