005-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuchunga (Kumukhofu Allaah Kwa Siri Na Dhahiri)

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب المراقبة

005 – Mlango Wa Kuchunga (Kukmhofu Allaah Kwa Siri Na Dhahiri)

 

Alhidaaya.com

 

 

  قَالَ الله تَعَالَى:

الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ

Ambaye Anakuona wakati unaposimama. [Ash-Shu’araa: 218]

 

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. [Al-Hadiyd: 4]

 

هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ

Je, hakuna katika hayo kiapo kwa mwenye welekevu (akawa na taqwa)? [Al-Fajr: 5]

 

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ

Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Awavizia. [Al-Fajr: 14]

 

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ

 (Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua. [Ghaafir: 19]

 

 

Hadiyth – 1

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: بَيْنَما نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَومٍ، إذْ طَلَعَ عَلَينا رَجُلٌ شَديدُ بَياضِ الثِّيابِ، شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيهِ أثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيهِ إِلَى رُكْبتَيهِ، وَوَضعَ كَفَّيهِ عَلَى فَخِذَيهِ.

وَقالَ: يَا مُحَمَّدُ، أخْبرني عَنِ الإسلامِ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ: أنْ تَشْهدَ أنْ لاَّ إلهَ إلاَّ الله وَأنَّ مُحمَّدًا رسولُ الله، وتُقيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ البَيتَ إن اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبيلًا)). قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقهُ!

قَالَ: فَأَخْبرنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَالَ: ((أنْ تُؤمِنَ باللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبهِ، وَرُسُلِهِ، وَاليَوْمِ الآخِر، وتُؤْمِنَ بالقَدَرِ خَيرِهِ وَشَرِّهِ)). قَالَ: صَدقت. قَالَ: فأَخْبرني عَنِ الإحْسَانِ. قَالَ: ((أنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاكَ)).

قَالَ: فَأَخْبِرني عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: ((مَا المَسْؤُولُ عَنْهَا بأعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ)). قَالَ: فأخبِرني عَنْ أمَاراتِهَا. قَالَ: ((أنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وأنْ تَرَى الحُفَاةَ العُرَاةَ العَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في البُنْيَانِ)).

ثُمَّ انْطَلقَ فَلَبِثْتُ مَلِيًّا، ثُمَّ قَالَ: ((يَا عُمَرُ، أَتَدْري مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ. قَالَ: ((فإنَّهُ جِبْريلُ أَتَاكُمْ يعْلِّمُكُمْ دِينَكُمْ)). رواه مسلم

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Rasuli) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislaamu.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  “Uislamu ni kukiri kuwa hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa  Allaah, na Muhammad ni Rasuli wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl): “Umesema kweli.” Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza  kwake Rasuli na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan.  Akasema: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na siku ya Qiyaamah, na  kuamini Qadar  (majaaliwa ya Allaah) ya kheri zake na shari zake.” (Akasema Jibriyl): “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.”  Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.”  Akasema (Jibriyl): “Niambie    kuhusu Qiyaamah.”  Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: “Nijulishe alama zake.”: Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Rasuli wake wanajua zaidi.  Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.” [Muslim]

 

Hadiyth – 2

عن أبي ذر جُنْدُب بنِ جُنادَةَ وأبي عبدِ الرحمنِ معاذِ بنِ جبلٍ رضي الله عنهما عن رسولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((اتَّقِ الله حَيْثُمَا كُنْتَ وَأتْبعِ السَّيِّئَةَ الحَسَنَةَ تَمْحُهَا، وَخَالِقِ النَّاسَ بِخُلُقٍ حَسَنٍ)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)

Abuu Dharr, Jundub bin Junaadah na Abuu ‘Abdir-Rahmaan Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mche Allaah popote ulipo, ufuatishe tendo jema baada ya tendo baya ili lifute, na utangamane na watu kwa tabia njema.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan]

 

Hadiyth – 3

عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: ((يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).

وفي رواية غيرِ الترمذي: ((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (juu ya mnyama). Akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema: “Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”

 

Hadiyth – 4

عن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: إِنَّكُمْ لَتعمَلُونَ أعْمَالًا هي أدَقُّ في أعيُنِكُمْ مِنَ الشَّعْرِ، كُنَّا نَعُدُّهَا عَلَى عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم مِنَ المُوبِقاتِ. رواه البخاري

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Kwa hakika ninyi mnafanya matendo ambayo machoni mwenu (mnayaona kuwa) ni madogo kulikoni unywele. Kwa hakika matendo hayo tulikuwa tukiyahesabu wakati wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni matendo yanayoangamiza.” [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 5

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الله تَعَالَى يَغَارُ، وَغَيرَةُ الله تَعَالَى، أنْ يَأتِيَ المَرْءُ مَا حَرَّمَ الله عَلَيهِ)). متفق عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hufanya ghera, na ghera ya Allaah ni mtu kutenda Aliyoharamisha Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 6

 عن أبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّه سَمِعَ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، يقُولُ: ((إنَّ ثَلاثَةً مِنْ بَني إِسْرَائِيلَ: أبْرَصَ، وَأَقْرَعَ، وَأَعْمَى، أَرَادَ اللهُ أنْ يَبْتَليَهُمْ فَبَعَثَ إِليْهمْ مَلَكًا، فَأَتَى الأَبْرَصَ، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إلَيْكَ؟ قَالَ: لَوْنٌ حَسنٌ، وَجِلدٌ حَسَنٌ، وَيَذْهبُ عَنِّي الَّذِي قَدْ قَذِرَنِي النَّاسُ؛ فَمَسَحَهُ فَذَهَبَ عَنْهُ قَذَرُهُ وَأُعْطِيَ لَونًا حَسنًا وجِلْدًا حَسَنًا. فَقَالَ: فَأيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليكَ؟ قَالَ: الإِبلُ- أَوْ قالَ: البَقَرُ شكَّ الرَّاوي- فَأُعطِيَ نَاقَةً عُشَرَاءَ، فَقَالَ: بَاركَ الله لَكَ فِيهَا. فَأَتَى الأَقْرَعَ، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إلَيْكَ؟ قَالَ: شَعْرٌ حَسَنٌ، وَيَذْهَبُ عَنِّي هَذَا الَّذِي قَذِرَني النَّاسُ؛ فَمَسَحَهُ فَذَهبَ عَنْهُ وأُعْطِيَ شَعرًا حَسَنًا. قالَ: فَأَيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليْكَ؟ قَالَ: البَقَرُ، فَأُعْطِيَ بَقَرَةً حَامِلًا، وَقالَ: بَارَكَ الله لَكَ فِيهَا.

فَأَتَى الأَعْمَى، فَقَالَ: أَيُّ شَيءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: أَنْ يَرُدَّ الله إِلَيَّ بَصَرِي فَأُبْصِرُ بِهِ النَّاسَ؛ فَمَسَحَهُ فَرَدَّ اللهُ إِلَيْهِ بَصَرهُ. قَالَ: فَأَيُّ المَالِ أَحَبُّ إِليْكَ؟ قَالَ: الغَنَمُ، فَأُعْطِيَ شَاةً والدًا، فَأَنْتَجَ هذَانِ وَوَلَّدَ هَذَا، فَكانَ لِهذَا وَادٍ مِنَ الإِبلِ، وَلِهذَا وَادٍ مِنَ البَقَرِ، وَلِهَذَا وَادٍ مِنَ الغَنَمِ.

ثُمَّ إنَّهُ أَتَى الأَبْرَصَ في صُورَتِهِ وَهَيئَتِهِ، فَقَالَ: رَجلٌ مِسْكينٌ قَدِ انقَطَعَتْ بِيَ الحِبَالُ في سَفَري فَلا بَلاغَ لِيَ اليَومَ إلا باللهِ ثُمَّ بِكَ، أَسْأَلُكَ بِالَّذي أعْطَاكَ اللَّونَ الحَسَنَ، والجِلْدَ الحَسَنَ، وَالمَالَ، بَعِيرًا أَتَبَلَّغُ بِهِ في سَفَري، فَقَالَ: الحُقُوقُ كثِيرةٌ. فَقَالَ: كأنِّي اعْرِفُكَ، أَلَمْ تَكُنْ أَبْرَصَ يَقْذَرُكَ النَّاسُ فقيرًا فأعْطَاكَ اللهُ!؟ فَقَالَ: إِنَّمَا وَرِثْتُ هَذَا المالَ كَابِرًا عَنْ كَابِرٍ، فَقَالَ: إنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ الله إِلَى مَا كُنْتَ.

وَأَتَى الأَقْرَعَ في صُورَتِهِ وَهَيْئَتِهِ، فَقَالَ لَهُ مِثْلَ مَا قَالَ لِهَذا، وَرَدَّ عَلَيهِ مِثْلَ مَا رَدَّ هَذَا، فَقَالَ: إنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ اللهُ إِلَى مَا كُنْتَ.

وَأَتَى الأَعْمَى في صُورَتِهِ وَهَيْئَتِهِ، فَقَالَ: رَجُلٌ مِسْكينٌ وابنُ سَبيلٍ انْقَطَعتْ بِيَ الحِبَالُ في سَفَرِي، فَلا بَلاَغَ لِيَ اليَومَ إلا بِاللهِ ثُمَّ بِكَ، أَسأَلُكَ بالَّذِي رَدَّ عَلَيْكَ بَصَركَ شَاةً أَتَبَلَّغُ بِهَا في سَفري؟ فَقَالَ: قَدْ كُنْتُ أعمَى فَرَدَّ اللهُ إِلَيَّ بَصَرِي فَخُذْ مَا شِئْتَ وَدَعْ مَا شِئْتَ فَوَ اللهِ لا أجْهَدُكَ اليَومَ بِشَيءٍ أخَذْتَهُ للهِ- عز وجل-. فَقَالَ: أمْسِكْ مالَكَ فِإنَّمَا ابْتُلِيتُمْ. فَقَدْ رضي الله عنك، وَسَخِطَ عَلَى صَاحِبَيكَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah Alitaka kuwapa mtihani watu watatu katika wana Israaiyl: Mwenye ukoma, mwenye kunyonyoka nywele (kipara) na kipofu. Akawapelekea Malaaika. Akamwendea mwenye ukoma. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda niwe na rangi nzuri, ngozi nzuri na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Yule Malaaika akampangusa, ukoma ukamuondokea na akapewa rangi na ngozi nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?”  Akajibu: “Ngamia.”. Au alisema: Ng’ombe, (mpokezi amekuwa na mashaka kama ni ng’ombe au ngamia). Akapewa ngamia mwenye mimba (karibu na kuzaa). Akamuombea: “Allaah Akubariki”.

Akamuendea mwenye upara. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Nywele nzuri, na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Akampangusa, akaondokewa na upara na akawa na nywele nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Ng’ombe.” Akapewa ng’ombe mwenye mimba. Akamuombea: “Allaah Akubarikie.” Akamuendea kipofu akamuuliza: “Kitu gani unachonapenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda Allaah Anirudishie macho yangu ili nione watu.” Akampangusa. Allaah Akamrudishia macho yake. Akamuuliza. “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Mbuzi.” Akapewa mbuzi mwenye mtoto. Wale wenye ngamia na ng’ombe wanyama wao wakazaa, na mwenye mbuzi nae akazalisha. Mmoja wao akawa na bonde lililojaa ngamia, na mwengine ana bonde lililojaa ng’ombe na huyu ana bonde lililojaa mbuzi. Kisha, akamuendea mwenye ukoma katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana nae kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Allaah kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekupa rangi nzuri, ngozi nzuri na mali, unipe ngamia ili nimalize safari yangu.” Akamjibu: “Haki zipo nyingi (nina majukumu mengi, kwa hiyo siwezi kukusaidia). Akamwambia: “Kana kwamba nakujua, si ulikuwa na ukoma na watu wanakudharau na ulikuwa fukara, na Allaah Akakupa?” Akamwambia: “Mali hii nimerithi kutoka kwa mababu na mababu.” Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea mwenye upara katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia kama alivyomwambia wa mwanzo. Naye akamrudishia jibu kama alivyomrudishia wa mwanzo. Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea kipofu katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Allaah kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekurudishia macho yako, unipe mbuzi ili nimalizie safari yangu.” Akamjibu: “Kwa hakika nilikuwa kipofu, Allaah Akanirudishia kuona kwangu. Chukua unachotaka, wacha unachotaka. Wa-Allaahi sikufanyia uzito kwa kitu ulichokichukua kwa Ajili ya Allaah.” Akamwambia “Zuia mali yako. Hakika mumepewa mtihani. Hakika Allaah Ameshakuridhia na Amewaghadhibikia wenzio wawili.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 7

عن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مِنْ حُسْنِ إسْلامِ المَرْءِ تَرْكُهُ مَا لا يَعْنِيهِ)). حديث حسن. رواه الترمذي وغيرُه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Katika uzuri wa Uislaamu wa mtu, ni kuacha lisilomuhusu.” [Hadiyth hii ni Hasan. At-Tirmidhiy na wengine]

 

Hadiyth – 8

عن عُمَرَ رضي الله عنه عَنِ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لا يُسْأَلُ الرَّجُلُ فِيمَ ضَرَبَ امْرَأَتَهُ)). رواه أبو داود وغيره

‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu haulizwi sababu ya kumpiga mkewe.” [Abuu Dawuud na wengineo]

 

 

 

 

 

 

 

 

Share