189-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 189: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah 189: Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi. Sema...

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾

189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.” Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka pale walipokuwa Answaar wa Madiynah wakienda Hajj na wakirejea wanapitia kwa nyuma ya majumba yao na hawakuwa wakiingia majumbani mwao kwa kupitia milango ya mbele ya majumba yao. Siku moja alikuja mtu mmoja akiwa ametoka Hajj akaingia kupitia mlango wa mbele wa nyumba yake akaaibishwa kwa ajili ya kitendo chake hicho. Hapo basi ikateremka Aayah hii. Hadiyth kama ilivyothibiti:

عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ ـ ر

ضى الله عنه ـ يَقُولُ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِينَا، كَانَتِ الأَنْصَارُ إِذَا حَجُّوا فَجَاءُوا لَمْ يَدْخُلُوا مِنْ قِبَلِ أَبْوَابِ بُيُوتِهِمْ، وَلَكِنْ مِنْ ظُهُورِهَا، فَجَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ، فَدَخَلَ مِنْ قِبَلِ بَابِهِ، فَكَأَنَّهُ عُيِّرَ بِذَلِكَ، فَنَزَلَتْ: ((‏وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَنْ تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ ظُهُورِهَا وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَى وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا‏))

Abuu Is-haaq amehadithia kwamba nilimsikia Al-Baraa akisema:  Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi, kwani Answaar walikuwa wanaporudi Hajj hawakuwa wakiingia majumbani mwao kupitia milango ya mbele bali wakiingia kwa milango ya nyuma. Akaja mtu katika Answaar akaingia kwa mbele, akatahayarishwa, ikateremka: Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake…”  [Al-Bukhaariy Kitaab Al-‘Umrah na Muslim Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

Share