28-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kumwendea kahini na mpiga ramli?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

28-Je, Inajuzu kumwendea kahini na mpiga ramli?

 

Hapana! Haijuzu kumwendea kahini wala mpiga ramli.

 

هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾

Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾

Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi.  [Ash-Shu’araa: 221-222]

 

((مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً)) مسلم

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]

 

 

 

 

 

Share