43-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameumbwa kutokana na nini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

43-Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na nini?

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na manii (kwa sababu yeye ni mwana Aadam kama sisi).

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone la manii. [Ghaafir: 67]

 

((إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه فِي أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً)) متفق عليه

((Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa manii)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Manii ni mbegu za uzazi za mama na baba.

 

Share