266-Aayah Na Mafunzo: Mfano Wa Tajiri Anayemuasi Allaah Mpaka Zikapotea ‘Amali Zake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mfano Wa Tajiri Anayemuasi Allaah Mpaka Zikapotea ‘Amali Zake

 

www.alhidaaya.com

 

 

 أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾

 

266. Je! Anapenda mmoja wenu awe ana bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya mazao; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (ishara, zingatio n.k) kwenu mpate kutafakari.

 

 

Mafunzo:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ،‏.‏ قَالَ وَسَمِعْتُ أَخَاهُ أَبَا بَكْرِ بْنَ أَبِي مُلَيْكَةَ، يُحَدِّثُ عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، قَالَ:  قَالَ عُمَرُ رضى الله عنه يَوْمًا لأَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم:  فِيمَ تَرَوْنَ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ ‏ ((أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَنْ تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ‏))‏ قَالُوا اللَّهُ أَعْلَمُ‏.‏ فَغَضِبَ عُمَرُ فَقَالَ: قُولُوا نَعْلَمُ أَوْ لاَ نَعْلَمُ‏.‏ فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فِي نَفْسِي مِنْهَا شَىْءٌ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ‏.‏ قَالَ عُمَرُ: يَا ابْنَ أَخِي قُلْ وَلاَ تَحْقِرْ نَفْسَكَ‏.‏ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: ضُرِبَتْ مَثَلاً لِعَمَلٍ‏.‏ قَالَ عُمَرُ أَىُّ عَمَلٍ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ لِعَمَلٍ‏.‏ قَالَ عُمَرُ: لِرَجُلٍ غَنِيٍّ يَعْمَلُ بِطَاعَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ، ثُمَّ بَعَثَ اللَّهُ لَهُ الشَّيْطَانَ فَعَمِلَ بِالْمَعَاصِي حَتَّى أَغْرَقَ أَعْمَالَهُ‏.‏ ‏(‏فَصُرْهُنَّ‏)‏ قَطِّعْهُنَّ‏.‏

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia kaka yake Abuu Bakr bin Abiy Mulaykah akihadithia kutoka kwa ‘Ubayd bin ‘Umayr kwamba: Siku moja ‘Umar (رضي الله عنه) aliwaambia Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Mnadhani Aayah hii imeteremka kwa ajili ya nani?” “Je, Anapenda mmoja wenu awe ana bustani…” Wakasema: “Allaah Ndiye Mjuzi.” ‘Umar akakasirika akasema: “Semeni tunajua au hatujui!.” Ibn ‘Abbaas akasema: Nimefikiri jambo katika nafsi yangu Ee Amiyrul-Muuminiyn.” ‘Umar akasema: “Ee mtoto wa ndugu yangu! Sema wala usiidharau nafsi yako.” Ibn ‘Abbaas akasema: “Imepigiwa mfano wa matendo.” ‘Umar akasema: “Matendo gani?” Ibn ‘Abbaas akasema: “Matendo.” ‘Umar akasema: “(Mfano) wa mtu tajiri anayemtii Allaah kisha Allaah Akamtumia shaytwaan, akafanya maasi mpaka ‘amali zake zote zikapotea” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share