279-Aayah Na Mafunzo: Anayeshughulika Na Ribaa Ajitangazie Vita Na Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Anayeshughulika Na Ribaa Ajitangazie Vita Na Allaah

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾

279. Na msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu basi mtapata rasilimali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe

 

Mafunzo:

 

Ilipoteremka Aayah Namba (2: 275) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema; “Yeyote asiyejizuia kufanya mukhaabarah (kukodisha shamba kwa malipo ya kugawana sehemu ya mazao) basi apokee tangazo la vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr] 

 

Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia: Alikuja Bilaal kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na aina ya tende nzuri. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Umetoa wapi hizi?” Akasema: Tulikuwa tuna tende mbaya nikaziuza pishi mbili kwa pishi moja (ya tende nzuri). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana! Hiyo ndiyo ribaa. Usifanye hivyo! Lakini ukitaka kununua basi uza tende zisizo nzuri kisha (kwa pesa) nunua tende nzuri kwa bei uliyopatia.” [Muslim]

 

Share