Fadhila Za Kumtembelea Mgonjwa

  Fadhila Za Kumtembelea Mgonjwa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

1. Kwanza Kabisa Ni Miongoni Mwa Haki Ya Muislamu Kwa Nduguye Muislamu

 

عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Haki ya Muislamu kwa nduguye Muislamu ni tano: Kujibu Salaam, kumtembelea mgonjwa, kulisindikiza jeneza, kuitikia mwito na kumuombea mwenye kupiga chafya)) [Al-Bukhaariy Muslim]

 

 

2. Siku Ya Qiyaamah Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atakuuliza

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي،  قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟  يَا ابْنَ آدَمَ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟  قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟  يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم

Kutoka Kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Aadam, Niliumwa na usije kunitembelea? Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa  ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye? Ee mwana wa Aadam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]  

 

 

3. Malaika Sabini Elfu Wanakuombea Rahmah 

 

Kumtembelea mgonjwa kuna fadhila nyingi tukufu kama zilivyothibiti katika Hadiyth kadhaa mojawapo ni kwamba mwenye kumtembelea mgonjwa huswaliwa na Malaika elfu sabini. Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا عَادَ الرَّجُلُ أَخَاهُ المُسْلِمَ مَشَى فِي خِرَافَةِ الجَنَّةِ حَتَّى يَجْلِسَ فَإِذَا جَلَسَ غَمَرَتْهُ الرَّحْمَةُ، فَإِنْ كَانَ غُدْوَةً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِيَ، وَإِنْ كَانَ مَسَاءً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبِحَ)).

Amesema (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mtu anapomtembelea ndugu yake Muislamu mgonjwa, basi hutembelea katika bustani ya Jannah mpaka atakapoketi, na anapoketi hufunikwa na Rahmah ikiwa ni asubuhi wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka jioni. Na ikiwa ni jioni wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka asubuhi)) [Swahiyh Ibn Maajah (1/244), Swahiyh At-Tirmidhiy (1/286)]

 

 

4. Du’aa Kutakabaliwa

 

Juu ya hivyo ni fursa kwa Muislamu kuomba du’aa yake itakabaliwe. Aanze kwanza kumwombea mgonjwa du’aa zilizothibiti katika Sunnah kisha ajiombee nafsi yake:

 

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رضي الله عنها)  قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا حَضَرْتُمْ الْمَرِيضَ أَوْ الْمَيِّتَ فَقُولُوا خَيْرًا فَإِنَّ الْملآئِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ أَتَيْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقُلْتُ:  يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سَلَمَةَ قَدْ مَاتَ قَالَ:  ((قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ وَأَعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبَى حَسَنَةً)) قَالَتْ: فَقُلْتُ فَأَعْقَبَنِي اللَّهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ مُحَمَّدًا (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnapohudhuria mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo mema kwani Malaika wanaitikia ‘Aamiyn’ msemayo)). Akasema: Alipofariki Abuu Salamah nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Abuu Salamah amefariki. Akasema: ((Sema: ‘Allaahumma-ghfir-liy wa lahu wa 'a-qibniy minhu ‘uqba hasanah’ [Ee Allaah, nighufurie pamoja naye na nilipie baada yake badali iliyo njema])). Akasema:  Akanilipa Allaah aliye mbora zaidi kuliko yeye; (ambaye ni) Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam))). [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

 

Share