238-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 238: حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 238: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati...

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.

 

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri)... imeteremka kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Alikuwa akiswali Swalaah ya Adhuhuri nusu ya mchana wakati jua linaposhtadi, na ilikuwa ni Swalaah ngumu zaidi kwa Swahaba (رضي الله عنهم). Mara nyingine ilikuwa haipatikani nyuma yake isipokuwa safu moja au mbili. Baada ya hali hiyo, ikateremka Aayah hii. [Ahmad kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu” ni kwamba, Swahaba walikuwa wakizungumza ndani ya Swalaah; mtu anamsemesha ndugu yake katika haja zake akiwa ndani ya Swalaah. Basi hapo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Zayd bin Arqam (رضي الله عنه)]

 

 

 

 

 

 

 

 

Share