024-Aayah Na Mafunzo: Haramisho La Ndoa Ya Mut’ah

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Haramisho La Ndoa Ya Mut’ah

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

Mafunzo:

 

Uharamisho wa ndoa ya mut’ah: Sabrah bin Ma’bad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Fat-hi Makkah akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut’ah amwache na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo].

 

 

 

Share