058-Aayah Na Mafunzo: Amri Ya Kurudisha Amana Kwa Mwenye Haki Nayo

 

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Amri Ya  Kurudisha Amana Kwa Mwenye Haki Nayo

Na Sababu Ya Kuteremshwa Aayah Hii

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Ni uzuri ulioje wa Anayokuwaidhini kwayo Allaah! Hakika Allaah daima ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote. [An-Nisaa: 58]

 

Mafunzo:

 

Umuhimu wa kuweka na kurudisha amana ya mtu:

 

Samurah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Rudisha amana kwa aliyekuaminisha na wala usimfanyie khiyana aliyekukhini.” [Ahmad, Swahiyh Abiy Daawuwd (3535), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (423)].

 

Sababun-Nuzuwl, Aayah Pekee Katika Suwrah hii Kuteremswa Makkah.

 

Aayah hii ni ya pekee katika Suwrah hii ya An-Nisaa (4:58) ambayo imeteremka Makkah. Imeteremshwa Siku ya Fat-h Makkah (Ushindi). Ibn Jurayj amehadithia kwamba imeteremshwa kuhusu ‘Uthmaan bin Twalhah pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipochukua ufunguo wa Ka’bah kutoka kwake akaingia Ka’bah. Alipotoka nje ya Ka’bah, alitoka huku akiwa anasoma:

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.”

 

Hapo akamwita ‘Uthmaan bin Twalhah na akampa funguo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]. Funguo hizo zimeendelea kubakia katika ukoo huo, kizazi baada ya kizazi mpaka sasa, na mpaka Siku ya Qiyaamah ukoo huo umefadhilishwa kuwa ndio wenye amana ya kukamata funguo za Al-Ka’bah.

 

 

 

 

 

Share