05-Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad: Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi Kuwa Na Swawm

Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi  Kuwa Na Swawm

 

Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, ni sharti mtu ili afanye I´tikaaf awe ana Swawm? 

 

 

JIBU:

Hapakudhihiri kitu kwangu kuwa ni sharti hilo (la mtu awe katika Swawm) kutokana na kufanya kwake (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) I´tikaaf siku kumi za Shawwaal, haikuthibiti kuwa alifunga. Hakuna kinachoonesha kuwa alifunga. 

 

 

[Bawaabah Al-Haramayn Ash-Shariyfayn]

 

 

Share