07-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Amemaliza Damu Ya Uzazi Kabla Ya Ramadhwaan Kisha Akaanza Swiyaam

Amemaliza Damu Ya Uzazi Kabla Ya Ramadhwaan Kisha Akaanza Swiyaam 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mke wangu alizaa mtoto kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhwaan baada ya siku saba alisafika (damu ya uzazi ikaisha) kabla ya kuingia Ramadhwaan. (Kisha akafunga Ramadhwaan) Je, funga yake imefaa au anatakiwa alipe siku hizo ingawa alifunga wakati alikuwa yuko katika twahaarah (ya damu ya uzazi)  Tafadhali tujulisheni. Allaah Akulipeni mema. 

 

 

JIBU:

 

Ikiwa hali ni kama ilivyoelezwa, basi swawm ya mke wako katika mwezi wa Ramadhwaan wakati yuko katika hali ya twahaarah (kukauka damu ya uzazi) inafaa na haimpasi kulipa siku hizo.

 

Na kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ndio yako mafanikio yote na Swalah na Salaam zimfikie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaaba zake.

 

 

[Halmashauri Ya Kudumu Ya Utafiti wa Kiislamu na Fataawaa inayoongozwa na:

Kiongozi Mkuu:  Shaykh 'Abdul-'Aziyz 'Abdillaah Ibn Baaz.

Msaidizi Kiongozi Mkuu:  Shaykh 'Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

Mwanachama: Shaykh 'Abdullah Ibn Ghudayyaan

 

Fataawa Ramadhwaan, Mjalada 2, Ukurasa 590, Fatwa Nambari 575.  Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa , Fatwa Nambari 10138

 

 

Nyongeza:

 

Hii ina maana kwamba si lazima mwanamke aliyezaa akamilishe siku 'arubaini ndio aweze kufunga au kuswali. Madamu kamaliza kutoka damu ya uzazi na ametwaharika, basi siku yoyote ile atakayotwaharika, inampasa afanye ghuslu (josho) kisha atimize ‘ibaadah zake kama kawaida.

 

 

Share