02-Imaam Ibn Baaz : Hakujua Kama Swawm Ilikuwa Fardhi Kwake; Je, Alipe Swawm Zilizompita?

Hakujua Kama Swawm Ilikuwa Fardhi Kwake; Je, Alipe Swawm Zilizompita?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Miaka kumi nyuma, nilifikia umri wa kubaleghe baada ya kuona alama zake.  Kwa hiyo mwaka wangu wa mwanzo wa ujana nimeacha Ramadhwaan imenipita na sikufunga bila ya kuwa na udhuru wowote, ila ni kwa sababu ya kutokujua kama ni fardhi wakati ule. Je, Inanipasa nilipe siku hizo na je, Inanipasa nifanye mengine juu yake kama kulipa kafara? 

 

 

JIBU:

 

Inakupasa ulipe siku zote zilizokupita za mwezi huo ambao hukuzifunga, na kuomba maghfirah na tawbah (Kwa Allaah Ta’aalaa) kisha ulipe kafara nayo ni nusu swaa' (nusu pishi sawa na vibaba viwili, ambayo ni sawa na 1.5kg) ya chakula kinacholiwa katika nchi hiyo kama tende, au mchele au chochote chengine kama unao uwezo. Kama wewe ni maskini na huna uwezo basi inatosha kama utafunga kulipa hizo siku usizofunga.

 

 

[Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk 559, Fatwa Namba 542; Al-Fataawaa libni Baaz - Kitaab Ad-Da'wah, Mj. 2, Uk. 158]

 

 

Share