17-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Du’aa "Allaahumma Balighnaa Ramadhwan", Haikuthibiti

 

Du’aa "Allaahumma Balighnaa Ramadhwan", Haikuthibiti

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Imaam aliulizwa kuhusu Hadiyth iliyotaja du’aa:

"اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان"

“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”

 

 

JIBU:

 

Hii ni dhaifu wala haikuthibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Na akasema tena Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah):

 

"Hakuna Hadiyth Sahihi ambayo inazungumzia fadhila za Rajab.

Mwezi wa Rajab hauna tofauti yeyote na mwezi wa Jumaadaa Al-Aakhirah ambao (ni mwezi) wa kabla yake, isipokuwa tu ni kuwa ni katika moja ya miezi mitukufu tu. Vinginevyo, hakuna Swawm iliyowekewa katika shariy'ah katika mwezi huu, na wala hakuna Swalaah au 'Umrah au chochote ambacho kimewekewa shariy'ah.

 

(Mwezi wa Rajab) ni kama miezi mingine tu.

 

[Liqaa Al-Baab Al-Maftuwh , 26/174]

 

Na katika sehemu nyingine anasema Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kuhusiana na khutbah hiyo:

 

"Mimi nawaambia (hali ya kuwa) nabainisha haki ya kuwa, mwezi wa Rajab hauna Swalaah maalum, si katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ndani yake na wala hauna Swawm katika siku ya kwanza ndani yake wala katika siku zilizobakia, bali uhakika ni kuwa (mwezi wa Rajab) ni kama miezi mingine kuhusiana na ufanyaji 'ibaadah, ijapokuwa ni mmoja kati ya miezi minne mitukufu.

 

Na wamejiliwaza na Hadiythi dhaifu zinazozungumzia kuihusu; kilichopokewa kwa Mtume kuwa alikuwa akisema inapoingia Mwezi wa Rajab:

"اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان"

“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”

 

Lakini hili enyi ndugu, sikilizeni ninayosema: Hii ni Hadiyth dhaifu munkar, haisihi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hivyo basi, hapaswi mtu kuomba du'aa hii kwa sababu haijasihi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

http://binothaimeen.net/content/5425

 

Share