Faida Na Hukmu Za Kuomba Tawbah - 02

 

Faida Na Hukmu Za Kuomba Tawbah - 02

 

Alhidaaya.com

 

 

Tunaendelea Kuzitaja Faida Za Kuomba Tawbah …

 

 

5-Kuwekewa Nuru (mwanga) Ambao Utamulika Wenye Kuomba Tawbah  Watakapokuwa Wanapita Katika Siraatw Siku Ya Qiyaamah:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَى رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ نُورُهُمْ يَسْعَى بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli); asaa Rabb   wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. [At-Tahriym: 8]

 

 

6-Malaika Wanawaombea Maghfirah Waumini Walioamini Na Wenye Kuomba Tawbah:

 

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾ 

(Malaika) Ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih kwa Himidi za Rabb wao, na wanamwamini; na wanawaombea maghfirah wale walioamini:  Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno. [Ghaafir: 7]

 

 

7- Kubadilishiwa Mabaya Na Kufanywa Yawe Mema: 

 

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴿٧٠﴾  

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Furqaan: 70]

 

Baada ya kujua faida nyingi na fadhila  za kuomba Tawbah, je, hustahiki ndugu Muislamu kupata  fadhila hizo adhimu? na nyingi nyinginezo? Kwanini usitubu ili uzipate? Asiyetaka kutubu baada ya kujua fadhila hizo ajue kuwa anajizuia na  kudhulumu nafsi yake kupata furaha, kufaulu duniani na akhera na pia kupata Ridhaa ya Rabb Wake.    

 

Bila shaka kila mmoja wetu atatamani fadhila hizo na kukimbilia kwa Rabb wetu kumuomba Tawbah ya Kweli. 

 

 

Inaendelea in Shaa Allaah...

 

Share