Al-Lajnah Ad-Daaimah: Uhakika Wa Ibn Taymiyyah Ni Ahlus-Sunnah Wal-Jam’aah

Uhakika Wa Ibn Taymiyyah Ni Ahlus-Sunnah Wal-Jam’aah

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Watu wanasema kwamba Ibn Taymiyyah alikuwa si mmoja katika Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah, na kwamba alipotea na kuwapotosha wengine, na kwamba hili ni kwa maoni ya Ibn Hajar na wengineo. Je, kwa hayo wanayoeleza ni kweli au la?

 

JIBU:

 

Shaykh Ahmad Ibn ‘Abdil-Haliym Ibn Taymiyyah ni mmoja wa Maimaam wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah ambaye aliwaita watu katika haki na katika njia sahihi. Allaah Aliisimamisha Sunnah kwa kumtumia yeye na kuwavunja nguvu wafuasi wa uzushi na uzushi na ukafiri.

 

Yule ambaye anamtambua kama ni mwengine zaidi ya hivyo ni yule ambaye ni mzushi na amepotea na anawapotosha wengine. Wamesikia mambo ya uongo kuhusiana naye, na wanafikiria kwamba ukweli ulikuwa ni uongo na uongo ulikuwa ni ukweli. Hayo yanatambuliwa na yule ambaye Allaah Anamuongoza na yule anayesoma kitabu chake na vitabu vya wapinzani wake, na kulinganisha wasifu wake na wao. Hii ni bora na ushahidi thabiti baina ya pande hizo mbili.

 

 

[Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Ibn Baaz, Shaykh ‘Abdur-Razzaaq ‘Afiyfiy, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Ghudayaan, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Qa’uwd. Fataawa Al-Lajnah Ad-Daa’imah (2/451, 254]. 

 

Share