Al-Lajnah Ad-Daaimah: Aashuraa: Kulipa Deni La Siwyaam Za Ramadhwaan Na ‘Aashuraa

 

Kulipa Deni La Siwyaam Za Ramadhwaan Na ‘Aashuraa

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah  

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Ambaye ana deni la Swawm ya mwezi wa Ramadhwaan kisha akataka kufunga Sunnah Swawm ya siku ya ‘Aashuraa yaani Swawm ya siku ya kumi na kumi na moja kwa niyyah ya kulipa na sio kufunga siku ya ‘Aashuraa ni nini hukumu yake? Na je inajuzu kufunga siku ya ‘Aashuraa kwa mwenye deni la Swawm ya Ramadhwaan? Na je inapasa kwa mwenye deni la Swawm ya Ramadhwaan kufunga siku ya ‘Aashuraa na siku kabla yake na siku baada yake kwa niyyah ya kulipa Ramadhwaan?

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLah.

 

Kwanza: Mtu hafungi Sunnah kama ana deni la Swawm ikiwa ni siku au masiku ya Ramadhwaan, bali mtu huyu ataanza kulipa Swawm ya deni ya Ramadhwaan na baada ya hapo atafunga Sunnah.

 

 

Pili: Akifunga siku ya kumi na kumi na moja katika mwezi wa Muharram kwa niyyah ya kulipa Swiyaam alizowacha za Ramadhwaan inajuzu hilo itakuwa amelipa siku mbili anazodaiwa kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  “Kwa hakika amali (za watu) zinahesibwa kwa niyyah, na kwa hakika kila mtu atahesabiwa kwa niyya yake.”

 

 

 Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaima Lil-Buhuwth Al-‘Ilmiyyah wal-Iftaai - Swali namba 67774].

 

 

 

Share