03-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah
03-Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah
عَنْ عُثْمَانَ بِنْ عَفَّان رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Afaan (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah ataingia Jannah)). [Muslim]