Kutokeza Baadhi Ya Nywele Za Mwanamke Kwenye Swalaah

 

 

 

Kutokeza Baadhi Ya Nywele Za Mwanamke Kwenye Swalaah Nini Hukmu Yake?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukumu ya swala ya mwanamke ambaye, keshamaliza swala, lakini baadaye akagundua kuwa sehemu ya nywele zake ndefu zilosukwa, zilikuwa zimetokeza nje?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Wanasema Wanachuoni, ikiwa sehemu ndogo ya nywele imetokeza na hakuwa akijua, basi hakuna juu yake chochote na Swalaah yake ni sahihi.

 

Hayo yamesemwa kwenye Al-Mughniy na vilevile Fataawa Nuwr 'Alaa Ad-Darb na hiyo ndio Fatwa ya Wanachuoni wengi.

 

 

Ama akiwa kwenye Swalaah akatambua kuwa kuna sehemu ndogo ya kiungo chake mtu kiko wazi basi akifunike haraka na Swalaah yake ni sahihi.

 

Wako Wanachuoni wanaoona ikiwa ni sehemu inayopasa kusitiriwa ipo wazi na muda mrefu umepita, basi Swalaah inabatilika. Kadhaalika wanaona ikiwa ni sehemu kubwa ya mwili iko wazi, basi Swalaah inabatilika.

 

Ama akifahamu hilo mtu baada ya Swalaah (kuwa kuna sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa wazi), basi wanaonelea Wanachuoni kuwa ni salama kuirudia ile Swalaah.

 

 

[Rejea, Fataawa Nuwr 'Alaa Ad-Darb, mj. 7, uk. 268]

 

 

Na Allaah ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share