Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Haijuzu Kusherehekea Valentine "Sikukuu Ya Wapenzi"

Haijuzu Kusherehekea Valentine "Sikukuu Ya Wapenzi"

 

Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Aliulizwa Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah): 

 

Kumeenea katika kipindi hiki cha mwisho kusherekea sikukuu ya kupendana haswa baina ya wanafunzi wa kike nayo ni sikukuu katika sikukuu za Manaswara. Na unakuwa (kwa kuvaa) vazi kamili jekundu; nguo viatu, na wanabadilishana (kupeana) maua mekundu. Tunataraji kutoka kwenu wabora kubainisha hukumu ya kusherekea mfano wa sikukuu hizi.

 

 

Akajibu Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah): 

 

Haijuzu kusherehekea Valentine kwa sababu (zifuatazo):

 

Kwanza: Hiyo ni sikukuu ya kizushi haina misingi katika shariy'ah
 
Pili: Hiyo (sikukuu) hulingania katika ashiki na mapenzi.
 
Tatu: Hiyo (sikukuu) hulingania katika kuushughulisha moyo kwa mambo yasiyokuwa na maana yanayoenda kinyume na njia ya wema waliopita.

 

Kwa hiyo, haifai kuzusha katika siku hii (ya Valentine) chochote katika nembo za sikukuu sawa sawa katika vyakula, au vinywaji, au mavazi, au kupeana zawadi au mengineyo yasiyokuwa hayo. Na inampasa Muislamu awe mtukufu (ajivune) kwa dini yake na wala asiwe mwenye kufuata mkumbo (akawa) anamfuata kila mwenye kuitia katika jambo la batili.
 
Na namuomba Allah awakinge Waislamu kutokana na kila fitnah (balaa) zilizo za dhahiri na zilizo jificha na Atusimamie kwa usimamizi Wake na Tawfiyq Yake.

 

 

[Fataawaa Al-‘Uthaymiyn (16/199)]

 

 

Share