046-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Al-A’raaf: Ukuta Wa Mwinuko

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 46

 

046-Maana Ya Al-A’raaf: Ukuta Wa Mwinuko

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾

Na baina yao kitakuwepo kizuizi. Na juu ya Al-A’raaf (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu watakaowatambua wote (wabaya na wema) kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: Salaamun ‘Alaykum!  Hawakuingia humo lakini bado wanatumaini. 

 

وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾

Na yatakapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa motoni watasema: Rabb wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.

 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾

Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari.

 

 أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾

Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah Hatowapa Rahmah yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika. 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾

Na watu wa motoni watawaita watu wa Jannah: Tumiminieni maji au katika ambavyo Amekuruzukuni Allaah. Watasema: Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.  [Al-A’raaf: 46-50]

 

 

Mafunzo:

 

Al-A’raaf:

 

Al-A’raaf ni Jina la Suwrah hii. Na Ibn ‘Abbaas, Ibn Mas’uwd, Ibn Jariyr na Salaf wengineo wamesema: Al-A’raaf ni sehemu watakayosimama watu ambao ‘amali zao njema na mbaya zimelingana sawasawa. ‘Amali zao ovu zimewazuia kuingia Jannah, na ‘amali zao njema zimewastahiki waepukane na moto. Kwa hiyo watasimamishwa hapo katika mnyanyuko wa Al-A’raaf mpaka Allaah Awahukumu. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share