054-Aayah Na Mafunzo: Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Kwa Siku Sita Na Maana Ya Istiwaa

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 54

 

054-Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Kwa Siku Sita Na Maana Ya Istiwaa

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾

Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa) ya ‘Arsh, Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi, na (Ameumba) jua na mwezi na nyota, (vyote) vimetiishwa kwa Amri Yake. Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu. [Al-A’raaf: 54]

 

 

Mafunzo:

 

 

Masiku Yaliyoumbwa Dunia Na Viliyomo:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah :(رضي الله عنه) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ)  Ameumba mchana siku ya Jumamosi, Akaumba milima Jumapili, Akaumba miti Jumatatu, Akaumba yanayochukiza Jumanne, Akaumba nuru Jumatano, kisha Akaeneza humo viumbe vinavyotembea Alkhamiys. Kisha Akamuumba Aadam (عليه السلام)  Ijumaa baada ya Alasiri. Alikuwa ni wa mwisho kuumbwa katika saa ya mwisho katika saa za Ijumaa, baina ya Alasiri na usiku.” [Ahmad]  

 

 

Maana ya Istawaa: Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah. Pia rejea tanbihi (2:29).

 

 

Share