17-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Kughufuriwa Makosa Japokuwa Ni Mfano Wa Povu La Bahari
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
17-Kughufuriwa Makosa Japokuwa Ni Mfano Wa Povu La Bahari
Akitamka mtu: “Laa ilaaha illa Allaah …” kila baada ya Swalaah baada ya Adkhaar za Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr mara thelathini na tatu kila moja na akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa Allaah…” mara moja:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((مَنْ سَبَّحَ اللَّهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَحَمِدَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَكَبَّرَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ وَقَالَ تَمَامَ الْمِائَةِ لا إِلَهَ إِلاّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakaye Sabbih (Subhaana Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu, akaleta tahmiyd (AlhamduliLLaah) mara thelathini na tatu akaleta takbiyra (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu] ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari)). [Muslim (1/418) [597]]