023-Riyaadhw As-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Riyaadhw As-Swaalihiyn

 

باب الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر

023 – Mlango Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ اللهُ تَعَالَى:

 

خَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. [Aal-‘Imraan: 104]

 

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari… [Aal-‘Imraan: 110]

 

 

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾

Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili. [Al-A’raaf: 199]

 

 

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wandani wao kwa wao, wanaamrisha mema na wanakataza munkari… [At-Tawbah: 71]

 

 

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani  ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya. [Al- Maaidah: 78-79]

 

 

وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ

Na sema: “Hii ni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru.” [Al-Kahf: 29]

 

 

فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿٩٤﴾

Basi tangaza wazi yale uliyoamrishwa na jitenge na washirikina. [Al-Hijr: 94]

 

 

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٥﴾

Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwaokoa wale wanaokataza uovu, na Tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki. [Al-A’raaf: 165]

 

 

 

Hadiyth – 1

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قَالَ: سَمِعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((مَنْ رَأى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ الإيمَانِ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Yoyote katika nyinyi atakayeona munkari na aubadilishe kwa mkono wake, na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa ulimi wake, na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa moyo wake, na huo ni udhaifu wa iymaan.” [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

عن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَا مِنْ نَبيٍّ بَعَثَهُ اللهُ في أمَّة قَبْلِي إلا كَانَ لَهُ مِنْ أُمَّتِهِ حَوَارِيُّونَ وَأصْحَابٌ يَأخُذُونَ بِسنَّتِهِ وَيَقْتَدُونَ بِأَمْرِهِ، ثُمَّ إِنَّهَا تَخْلُفُ مِنْ بَعْدِهِمْ خُلُوفٌ يَقُولُونَ مَا لا يَفْعَلُونَ وَيَفْعَلُونَ مَا لا يُؤْمَرونَ، فَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِيَدِهِ فَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِقَلبِهِ فَهُوَ مُؤمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِلسَانِهِ فَهُوَ مُؤمِنٌ، وَلَيسَ وَرَاءَ ذلِكَ مِنَ الإيمَانِ حَبَّةُ خَرْدَل)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakuna Nabiy yoyote aliyetumwa kabla yangu isipokuwa alikuwa na wateule wake (Maswahaba na wanafunzi wake) katika Ummah wake. Hawa Maswahaba (wa Manabiy) walikuwa wakifuata mwendo wake (Sunnah za Nabiy wao) na kufuata maagizo yake. Baada yao wakaja wafuasi waliozua (mambo yao wenyewe) huku wakisema wasiyotenda na kutenda wasiyoamrishwa. Hivyo, yoyote atakayepigana nao kwa mkono wake ni Muumin, na anayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumin, na anayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumin. Hapana nyuma ya haya chembe ya iymaan.” [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 3

عن أبي الوليدِ عبادة بن الصامِت رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْنَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى السَّمْعِ والطَّاعَةِ في العُسْرِ واليُسْرِ، والمَنْشَطِ وَالمَكْرَهِ، وَعَلَى أثَرَةٍ عَلَيْنَا، وَعَلَى أنْ لا نُنازِعَ الأمْرَ أهْلَهُ إلا أنْ تَرَوْا كُفْرًا بَوَاحًا عِنْدَكُمْ مِنَ اللهِ تَعَالَى فِيهِ بُرْهَانٌ، وَعَلَى أنْ نَقُولَ بالحَقِّ أيْنَمَا كُنَّا لا نَخَافُ في اللهِ لَوْمَةَ لاَئِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imeokewa kutoka kwa Abul Waliyd ‘Ubadah bin As-Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Tulimbay’ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) juu ya kusikia na kutii wakati wa mazito na mepesi, na katika raha na shida na kuweza kuhimilia wakati unapobaguliwa (na kushinda). Na pia tusiwe ni wenye kuzozana na viongozi isipokuwa unapoona ukafiri wa wazi kabisa, hapo mtakuwa na dalili ya wazi na ruhusa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Na tuwe ni wenye kusema kweli popote tulipo wala tusiogope lawama ya anaye laumu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 4

عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَثَلُ القَائِمِ في حُدُودِ اللهِ وَالوَاقعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَومٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ فَصَارَ بَعْضُهُمْ أعْلاها وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، وَكَانَ الَّذِينَ في أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقهُمْ، فَقَالُوا: لَوْ أنَّا خَرَقْنَا في نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤذِ مَنْ فَوقَنَا، فَإِنْ تَرَكُوهُمْ وَمَا أرَادُوا هَلَكُوا جَميعًا، وَإنْ أخَذُوا عَلَى أيدِيهِمْ نَجَوا وَنَجَوْا جَميعًا)). رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mfano wa mwenye kusimama juu ya mipaka ya Allaah (kwa kumtii) ni wale walioingia ndani (wenye kupuuza mipaka Yake), ni mfano wa watu walioshindana (kuingia) katika Safina, baadhi yao wakawa juu ya wengine wakawa katika sehemu ya chini. Ama kwa wale waliokuwa chini walipokuwa wanataka maji ya kunywa iliwabidi wapande juu, hivyo wakasema: Lau sisi tukitoboa tundu katika sehemu yetu hii ya chini hatutokuwa ni wenye kuwaudhi wa juu. Ikiwa wataacha wafanye wanayoyataka basi wataangamia wote na wakiwashika mikono yao basi wataokoka wao na wote kwa pamoja.” [Al- Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 5

عن أُمِّ المؤمنين أم سلمة هند بنت أَبي أمية حذيفة رضي الله عنها، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم أنه قَالَ: ((إنَّهُ يُسْتَعْمَلُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ فَتَعرِفُونَ وتُنْكِرُونَ، فَمَنْ كَرِهَ فَقَدْ بَرِئَ، وَمَنْ أنْكَرَ فَقَدْ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ)) قَالوا: يَا رَسُول اللهِ، ألا نُقَاتِلهم؟ قَالَ: ((لا، مَا أَقَامُوا فيكُمُ الصَّلاةَ)). رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummu Salamah Hind bint Abu Umayyah Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakika kutakuwa na watu watakaochaguliwa kama viongozi wenu, mtawajua na kuwachukia, yoyote atakayechukia atakuwa hana makosa, na yoyote atayechukia atakuwa hakika amesalimika, lakini (mwenye makosa) ni yule anayeridhika na akafuata.” Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tusipiganae nao? Akasema: “Msipigane nao, maadamu wataendelea kusimamisha Swalaah miongoni mwenu.” [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 6

عن أم المؤمنين أم الحكم زينب بنتِ جحش رَضِي الله عنها: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا فَزِعًا، يقول: ((لا إلهَ إلا الله، وَيلٌ للْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ اليَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأجُوجَ وَمَأجُوجَ مِثلَ هذِهِ))، وحلّق بأُصبُعيهِ الإبهامِ والتي تليها، فقلتُ: يَا رَسُول الله، أنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummul Hakam Zaynab bint Jahsh (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) aliingia kwake akiwa amefadhaika, akasema: “Hapana anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Ole wao Waarabu! kwa shari iliyokaribia. Imefunguliwa leo tundu katika ukuta unaowazuia Juwj na Ma-ajuwj mfano huo (na akachora duara kwa kutumia kidole gumba na kile kinachofuata).” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tutaangamizwa na miongoni mwetu kuna watu wema? Akasema: “Ndio, pindi maovu yatakapokithiri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 7

عن أَبي سعيد الخُدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إيَّاكُمْ وَالجُلُوسَ في الطُّرُقَاتِ!)) فقالوا: يَا رَسُول الله، مَا لنا مِنْ مجالِسِنا بُدٌّ، نتحدث فِيهَا. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((فَإذَا أبَيْتُمْ إلا المَجْلِسَ، فَأَعْطُوا الطَّريقَ حَقَّهُ)). قالوا: وما حَقُّ الطَّريقِ يَا رسولَ الله؟ قَالَ: ((غَضُّ البَصَرِ، وَكَفُّ الأَذَى، وَرَدُّ السَّلامِ، وَالأمْرُ بِالمَعْرُوفِ، والنَّهيُ عن المُنْكَرِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Nawatahadharisha nyinyi kwa kukaa kwenu njiani” Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hatuna budi isipokuwa kukaa (katika sehemu hizo) kwani tunazungumza na kujadiliana ndani yake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) “Ikiwa ni hivyo basi ipatieni njia haki yake” Wakasema: Ni zipi haki za njia Ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Kuinamisha macho chini, na kuondoka uchafu (pingamizi), na kurudisha salamu, na kuamrisha mema na kukataza maovu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 8

عن ابن عباس رضي الله عنهما: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم رأى خاتَمًا مِنْ ذهبٍ في يدِ رجلٍ فنَزعه فطرحه، وَقالَ: ((يَعْمدُ أحَدُكُمْ إِلَى جَمْرَةٍ مِنْ نَارٍ فَيَجْعَلُهَا في يَدِهِ!)) فقِيلَ لِلرَّجُلِ بَعْدَمَا ذهب رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم: خُذْ خَاتَمَكَ انْتَفِعْ بِهِ. قَالَ: لا والله لا آخُذُهُ أبَدًا وَقَدْ طَرَحَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم. رواه مسلم

Imepokewa na ibn ‘Abbas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimuona mtu amevaa pete ya dhahabu mkononi mwake. Alimtoa katika kidole chake na kuitupa. Kisha Akasema: “Mmoja wenu anakusudia kuliweka kaa la moto katika mkono wake!” Akaambiwa yule mtu baada ya kuondoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). Ichukue pete yako na ufaidike nayo. Akasema: Hapana! Naapa kwa Allaah, siichukui milele baada ya kutupwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 9

عن أَبي سعيد الحسن البصري: أن عائِذَ بن عمرو رضي الله عنه دخل عَلَى عُبَيْدِ اللهِ بنِ زياد، فَقَالَ: أي بُنَيَّ، إني سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول: ((إنَّ شَرَّ الرِّعَاءِ الحُطَمَةُ)) فَإِيَّاكَ أنْ تَكُونَ مِنْهُمْ، فَقَالَ لَهُ: اجلِسْ فَإِنَّمَا أنْتَ مِنْ نُخَالَةِ أصْحَابِ مُحَمَّد صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: وهل كَانَتْ لَهُم نُخَالَةٌ إِنَّمَا كَانَتِ النُّخَالَةُ بَعْدَهُمْ وَفي غَيْرِهِمْ. رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Hasan Al-Baswariy ya kwamba: ‘Aa’idh bin ‘Amru (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimtembelea ‘Ubaydullaah bin Ziyaad na kumwambia: Ewe mtoto wangu! hakika nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Hakika viongozi wabaya kabisa ni wale wakali (kwa raia wao). Hivyo, kuwa na tahadhari usiwe miongoni mwao.” Kaa chini kwani wewe ni miongoni mwa kumvi wa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). Akasema: (‘Aa’idh) na je, yeye alikuwa na kapi, hakika kumvi walikuja baada yao na watu wengine wasiokuwa wao. [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 10

عن حذيفة رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((وَالَّذِي نَفْسي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بِالمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ المُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللهُ أنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْهُ ثُمَّ تَدْعُوْنَهُ فَلا يُسْتَجَابُ لَكُمْ)). رواه الترمذي

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi Mwake, mtaendelea kuamrisha mema na kukataza maovu au kama si hivyo basi Allaah Atawateremshia adhabu, kisha mtamuomba yeye kisha hatawojibu (du’aa zenu).” [At-Tirmidhiy]

 

 

 

Hadiyth – 11

عن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أفْضَلُ الجِهَادِ كَلِمَةُ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائرٍ)). رواه أَبُو داود والترمذي

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jihadi iliyo bora kabisa ni kuzungumza maneno ya haki mbele ya kiongozi mjeuri.” [Abu Daawuwd na At-Tarmidhiy]

 

 

 

Hadiyth – 12

عن أَبي عبدِ الله طارِقِ بن شِهاب البَجَليِّ الأَحْمَسِيّ رضي الله عنه: أنَّ رجلًا سأل النَّبيّ صلى الله عليه وسلم وقد وضع رِجله في الغَرْزِ: أيُّ الجِهادِ أفضلُ؟ قَالَ: ((كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائرٍ)). رواه النسائي

Imepokewa kutoka kwa Abu ‘Abdillaah Twaariq bin Shihaab Al-Bajaliy Al-Ahmasiy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba, mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa tayari ameweka mguu kwenye kipandio cha Ngozi (au kibao) cha ngamia akasema: Ni Jihadi gani iliyobora kabisa? Akasema: “Kuzungumza maneno ya haki mbele ya kiongozi mjeuri.” [An-Nasaaiy]

 

 

 

Hadiyth – 13

عن ابن مسعود رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ أوَّلَ مَا دَخَلَ النَّقْصُ عَلَى بَنِي إسْرَائِيلَ أنَّهُ كَانَ الرَّجُلُ يَلْقَى الرَّجُلَ، فَيَقُولُ: يَا هَذَا، اتَّقِ الله ودَعْ مَا تَصْنَعُ، فَإِنَّهُ لاَ يَحِلُّ لَكَ، ثُمَّ يَلْقَاهُ مِنَ الغَدِ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ، فَلا يَمْنَعُهُ ذلِكَ أنْ يَكُونَ أكِيلَهُ وَشَرِيبَهُ وَقَعِيدَهُ، فَلَمَّا فَعَلُوا ذلِكَ ضَرَبَ اللهُ قُلُوبَ بَعْضِهِمْ بِبَعْضٍ)) ثُمَّ قَالَ: {لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرائيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُدَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ * كَانُوا لا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ * تَرَى كَثِيرًا مِنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ} إِلَى قوله: {فاسِقُونَ} [المائدة: 78- 81].

ثُمَّ قَالَ: ((كَلا، وَاللهِ لَتَأمُرُنَّ بالمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، وَلَتَأخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، وَلَتَأطِرُنَّهُ عَلَى الحَقِّ أَطْرًا، وَلَتَقْصُرُنَّه عَلَى الحَقِّ قَصْرًا، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللهُ بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنَنَّكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ)). رواه أَبُو داود والترمذي

هَذَا لفظ أَبي داود، ولفظ الترمذي، قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لَمَّا وَقَعَتْ بَنُو إسْرَائِيلَ في المَعَاصي نَهَتْهُمْ عُلَمَاؤهُمْ فَلَمْ يَنْتَهُوا، فَجَالَسُوهُمْ في مَجَالِسِهمْ، وَوَاكَلُوهُمْ وَشَارَبُوهُمْ، فَضَربَ اللهُ قُلُوبَ بَعضِهِمْ بِبعْضٍ، وَلَعَنَهُمْ عَلَى لِسانِ دَاوُد وعِيسَى ابنِ مَرْيَمَ ذلِكَ بما عَصَوا وَكَانُوا يَعتَدُونَ)) فَجَلَسَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وكان مُتَّكِئًا، فَقَالَ: ((لا، والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى تَأطِرُوهُمْ عَلَى الحَقِّ أطْرًا)).

Imepokewa kutoka kwa ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Upungufu wa kwanza uliowafikia Banuu Israiyl ulikuwa mtu kukutana na mwenzake, akimwambia: Ewe fulani! mche Allaah na uache unayofanya kwani si halali kwako (kufanya hivyo). Kisha anakutana naye siku ya pili katika hali yake ya awali (bila ya mabadiliko), hilo halimkatazi yeye kutokula naye, kunywa na kukaa naye. Walipofanya hivyo, Allaah Alibadilisha mioyo yao baadhi yao kwa wengine.” Kisha akasema: “Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani (lugha) ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.” Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.” “Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, ndipo Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.” “Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.” [Al-Maaidah: 78-81]

Kisha akasema: “Hasha! Naapa kwa Allaah ya kwamba mtaendelea kuamrisha mema na kukataza maovu na kuushika mkono wa dhalimu na kuwashawishi (kwa upole na ulaini) wafanye uadilifu, kuwafanya wawe imara juu ya haki na ukweli. Mkishindwa kufanya hivyo, basi jueni ya kwamba Allaah Atawaadhibu pamoja na wenzenu (madhalimu wa nafsi zao) na kisha Atawalaani kama Alivyowalaani wao (Mayahudi).” [Hii ni lafdhi ya Abu Daawuwd]

 

Riwaayah ya At-Tirmidhiy: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Walipoingia Banuu Israiyl katika maasi, Wanachuoni wao waliwakataza lakini hawakuacha, hivyo wakaanza kukaa nao katika baraza zao na wakawa wanakula na kunywa pamoja nao. Hapo Allaah Aliwaadhibu wote pamoja na wakalaaniwa kwa ulimi wa Dawwuud na ‘Iysaa bin Maryam na hiyo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka.”

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa baada ya kuwa ameegemea, kisha akasema: “Laa sivyo hivyo, naapa kwa Yule ambaye kwamba nafsi yangu ipo mikononi Mwake, mpaka muwashike mkono madhalimu ili waweze kusimama juu ya haki.” [At-Tirmidhiy]

 

 

 

Hadiyth – 14

عن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه قَالَ: يَا أيّها النَّاس، إنّكم لتَقرؤُون هذِهِ الآية: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ لا يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ} [المائدة: 105].

وإني سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوُا الظَّالِمَ فَلَمْ يأخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أوشَكَ أنْ يَعُمَّهُمُ اللهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ)). رواه أَبُو داود والترمذي والنسائي

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakr As-Swidiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ya kwamba alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma Aayah hii: “Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka.” Kwa hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika pindi watu wanapomuona dhalimu na wasimshike mikoni yake, huenda Allaah kwa ujumla akawateremshia adhabu kutoka Kwake.” [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

 

Share