Swalah Inavyoswaliwa Wakati Uko Safarini

 

 

SWALI:

ASSALAAMU ALAYKUM   NDUGU ZANGU,

ALHAMDULILLAH TANGU KUPATA   KWA  REHEMA YA ALLAH(S.W,T.)  HII WEB SITE NIMEFADIKA SANA NA NIMEPATA MAJIBU YA MASWALA  MENGI   YALIYYO KUWA YAKINI  HANGAISHA.NIME SOMA HABARI YA SWALAH YA SAFARI    LAKINI KUNA  SWALA MOJA   AMBAYO SIKU PATA MAJIBU  NDANI  YA TEXT HIYO.

 SWALI  NI:   JEE IKIWA TUNASAFIRI   KUTOKA   AFRICA KUJA  AMERICA KWA NDEGE  NI MUDA MREFU  NA SWALAH   KAMA 2 AU 3  ZINATUPITA. NAOMBA NISAIDIWE MWONGOZO. 

JAZAAKALLAHUKHEIR     BAARAKALLAHU FIIHI  FIAMANILLAH

 


 

 JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukran kwa swali lako zuri na muhimu sana hasa katika nyakati za sasa ambapo safari zimekuwa nyingi. Watu wengi wanasafiri baina nchi hadi nchi nyengine. Nyakati baina hizi dola zinatofautiana kwa kiai kikubwa.

Mbali na yote hayo ifahamike kuwa hakuna udhuru wa kuacha Swalah. Mtu anaweza kuchelewa kwa sababu zinazokubalika katika sheria, nazo ni kusahau, kulala, kujumuisha baina ya walah mbili mtu akiwa katika safari, kutotambua kuwa wakati wa Swalah umeingia mpaka ukatoka na kadhalika.

Jambo la muhimu la kufanya kwa sababu wewe uko katika safari hufai kuacha Swalah ikakupita. Allah Aliyetukuka Ametuonea huruma tukiwa katika hali hiyo kuwa tunaweza kuswali Swalah ya safari na kupunguza. Kwa mfano umeingia katika ndege na ipo angani, zipo ndege nyingine ambazo wametenga sehemu za kuswalia, hivyo wakati ukifika mtaswali ndani. Ikiwa hakuna sehemu iliyotengwa basi utajaribu kutafuta Qiblah na kuelekea pale ambapo una yakini kuwa ndipo sehemu ya Qiblah. Katika hali hiyo utaswali kwa kuketi. Ndege zinazomilikiwa na nchi za Kiislamu aghlabu yao huweka alama ya Qiblah. Na kama hukupata alama ya Qiblah basi utaswali kuelekea upande huo huo unaolekea. 

Mfano umetoka asubuhi na Swalah ya Adhuhuri imekukuta ukiwa angani na pengine pia Swalah ya Alasiri, hivyo unaweza kuchagua kuswali ima Swalah zote mbili wakati wa Adhuhuri au zote mbili wakati wa Alasiri. Utakavyoswali katika nyakati hizo mbili, utaswali rakaa mbili kisha utatoa salamu na kuswali nyingine mbili. Na Swalah ya Maghrib na ‘Ishaa pia unazichanganya lakini Swalah ya Maghrib utaswali vile vile rakaa tatu bila kupunguza na ya ‘Ishaa utaswali mbili.

Kwa manufaa na maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:

Safari-Mgonjwa

Na Allah Anajua zaidi 

 

Share