Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ramadhwaan: Mashaytwaan Kufungwa Minyororo Ilhali Waislamu Hutenda Maasi

 

Mashaytwaan Kufungwa Minyororo Ilhali Waislamu Hutenda Maasi

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inasema mashaytwaan hufungwa pingu na kutiwa minyororo katika mwezi huu lakini pamoja na hayo tunawaona watu wakipandwa na mashaytwaan na pia wakimwasi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mchana wa mwezi huu? Vipi mashaytwaan watiwe minyororo na baadhi ya watu waendelee kupandwa na mashaytwaan na kuasi?”

 

 

JIBU:

 

Yaliyotajwa katika Hadiyth hii ni mambo ya ghayb. Wajibu wetu sisi ni kuyasadiki, kuyakubali na kutojaribu kuzungumzia yaliyo nyuma yake. Hivi kunakuwa ni salama zaidi kwa Dini ya mtu na salama zaidi kwa khatima yake.

 

 

[Majmuw’ Fataawaa  (20)]

 

 

Share